DRE CALI ATIMKIA CANADA BAADA YA KUZICHAPA NA BOSI WAKE YKEE BENDA

DRE CALI ATIMKIA CANADA BAADA YA KUZICHAPA NA BOSI WAKE YKEE BENDA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda, Dre Cali ameripotiwa kutimkia nchini Canada baada ya kuzichapa na msanii Ykee Benda ambaye ni bosi wa lebo ya muziki ya Mpaka Records inayosimamia kazi zake za muziki. Inadaiwa wawili hao walirushiana makonde baada ya kuingia kwenye ugomvi mkali wa pesa, jambo lilompelekea Dre Cali kwenda mafichoni nchini Canada kwa ajili ya usalama wake. Chanzo cha karibu na Dre Cali kimeuambia mtandao wa Howwe kuwa msanii huyo alidanganya kuwa anasafiri nchini Canada kufanya shows hadi akapewa hatia ya usafiri ya miaka 10 ila kiuhalisia lengo lake kuu lilikuwa apate visa ya kwenda mafichoni. Utakumbuka Dre. Cali pia anaandamwa na msala mwingine wa kukiuka mkataba wake wa miaka 5 na menejimenti yake ya zamani ya “Wyse Technologies Limited” mwaka 2018 kabla ya kuijiunga na lebo ya “Mpaka Records” inayomilikiwa na msanii Ykee Benda. Kwa sasa uongozi wake wa zamani “Wyse Technologies Limited” unamtaka Dre Cali alipe fidia ya Shillingi laki 8 za Kenya kwa hasara aliyoiletea menejimenti yake hiyo huku ikisisitiza kuwa haitalegeza msimamo wake hadi pale watakapopata haki mahakamani.

Read More
 DRE CALI HATIANI KWA KUKIUKA MKATABA WAKE NA WYSE TECHNOLOGIES LIMITED

DRE CALI HATIANI KWA KUKIUKA MKATABA WAKE NA WYSE TECHNOLOGIES LIMITED

MMsanii wa Mpaka Records Dre Cali yuko matatani baada ya uongozi wake wa zamani wa Wyse Technologies Limited kutishia kufungulia mashtaka kwa kukiuka mkataba wa maelewano. Kulingana na barua na kutoka kwa Wyse Technologies, Dre Cali anaripotiwa kukiuka mkataba wa miaka 5 ambao alikubaliana na uongozi wake huo kwa lengo la kukuza kipaji chake cha muziki. Barua hiyo, inasema kwamba Dre Cali, ambaye kwa wakati huo alikuwa anaitwa ‘Drey 23’, alitia saini kandarasi hiyo ambayo ingedumu kwa kipindi chaΒ  miaka mitano kuanzia Machi 27, 2018 hadi Machi 27, 2023. Barua hiyo iliendelea kusomeka kuwa akiwa amekaa takribani miezi mitano tu chini ya uongozi wake wa zamani , Dre aliachana na uongozi huo na kujiunga na lebo ya Mpaka Records bila kufuata taratibu stahiki Kulingana na duru za kuaminika, Wyse technologies imemtaka Dre Cali kuwalipa takriban shillingi laki nane kama fidia.

Read More