Parroty Vunulu Aomba Msamaha kwa Kukataa Kunyoa Dreadlocks Zake Baada ya Manchester United Kupoteza

Parroty Vunulu Aomba Msamaha kwa Kukataa Kunyoa Dreadlocks Zake Baada ya Manchester United Kupoteza

Msanii wa Gengetone nchini Kenya, Parroty Vunulu, ameomba radhi kwa mashabiki na umma baada ya kutotimiza ahadi yake ya kunyoa rasta zake iwapo klabu ya Manchester United ingepoteza mechi dhidi ya Tottenham Hotspur. Parroty, ambaye alikuwa ameapa kunyoa dreadlocks zake alizozilea kwa miaka tisa endapo United wangeshindwa, amebadili msimamo wake na kusema hawezi kupoteza utambulisho wake kwa sababu ya matokeo ya mpira. “Heri niache kusupport Manchester United lakini nisipoteze image yangu,” alisema Parroty katika ujumbe aliouweka mitandaoni, akichanganya ucheshi na ukweli kuhusu uamuzi wake wa kutokata nywele hizo. Akiendelea kueleza sababu za kubadili uamuzi wake, Parroty alisema kuwa dreadlocks hizo ni sehemu muhimu ya chapa yake ya kisanii na kimtindo, na kwamba kunyoa nywele hizo kungemgharimu shughuli nyingi za kibiashara. “Nawaomba mashabiki wanielewe. Hizi rasta ndizo zimenitambulisha kwenye game, na kwa kweli zimenisaidia sana kibiashara. Nikizikata, ni kama najifuta kwenye ramani ya muziki,” aliongeza Parroty. Msanii huyo pia alifichua kuwa ana mpango wa kuandaa sherehe maalum ya kusherehekea miaka tisa ya kulea dreadlocks zake mwezi Septemba, kama njia ya kutambua safari yake ya kipekee ya mitindo ya nywele na kujieleza kisanii. “Niko na plan ya birthday kali Septemba. Sitaki tu kusherehekea siku yangu ya kuzaliwa, bali pia juhudi za kulea hizi rasta kwa miaka yote hii,” alisema kwa msisimko. Wakati baadhi ya mashabiki walichukulia hali hiyo kwa utani, wengine walimkumbusha umuhimu wa kushikilia ahadi. Hata hivyo, wengi walionekana kuelewa msimamo wake, wakitambua umuhimu wa muonekano katika kazi yake ya sanaa. Parroty Vunulu anaendelea kuwa mmoja wa wasanii wa Gengetone wanaovutia kutokana na ubunifu, ucheshi na uaminifu kwa mtindo wake wa maisha.

Read More
 Msanii wa Gengetone Parroty Aahidi Kunyoa Rasta Zake Iwapo Man U Itapigwa Usiku wa Leo

Msanii wa Gengetone Parroty Aahidi Kunyoa Rasta Zake Iwapo Man U Itapigwa Usiku wa Leo

Msanii maarufu wa Gengetone, Parroty, amezua gumzo mitandaoni baada ya kutoa ahadi ya kushangaza kupitia Instagram Live yake. Parroty alisema kuwa yuko tayari kunyoa dreadlocks zake alizozilea kwa miaka tisa endapo timu yake pendwa, Manchester United, itashindwa na Tottenham Hotspur katika mechi ya leo usiku. Kupitia matangazo ya moja kwa moja, Parroty alionekana kuwa na msimamo mkali kuhusu mechi hiyo, akisema: “Kama Man U itapigwa leo na Tottenham, basi na mimi nitanyoa hizi rasta mara moja!” Kauli hiyo imewavutia mashabiki wengi wa soka na muziki, huku baadhi wakimshabikia kwa ujasiri wake na wengine wakimkumbusha kuwa Tottenham si timu ya kubeza. Wengi sasa wanasubiri kwa hamu matokeo ya mechi hiyo ili kuona kama Parroty atatimiza ahadi yake. Mechi hiyo inatarajiwa kuwa ya kusisimua, huku macho ya mashabiki wa muziki na soka yakielekezwa kwa Parroty na hatima ya dreadlocks zake za miaka tisa.

Read More
 Bahati Awashukuru Mashabiki kwa Kumpongeza kwa Muonekano Mpya Licha ya Video Kuzua Maswali

Bahati Awashukuru Mashabiki kwa Kumpongeza kwa Muonekano Mpya Licha ya Video Kuzua Maswali

Mwanamuziki wa Kenya, Bahati, amezua gumzo mitandaoni baada ya kuwashukuru mashabiki wake kwa pongezi walizompa kuhusu muonekano wake mpya bila nywele. Kupitia video aliyochapisha kwenye kurasa zake za mitandao ya kijamii, Bahati alidai kuwa alinyoa rasta zake kufuatia kichapo cha timu yake ya Arsenal mikononi mwa PSG, katika mechi ya hivi karibuni ya UEFA Champions League. Katika ujumbe wake kwa mashabiki, Bahati alisema: “Nimeanza kujipenda zaidi bila nywele. Nimejifunza kuwa upendo wa kweli huanza na wewe mwenyewe.” Hata hivyo, kilichozua utata ni ubora wa video hiyo, ambayo inaonyesha mabadiliko ya haraka ya uhariri (transition), huku dreadlocks zake zikiendelea kuonekana kwa vipindi tofauti ndani ya video hiyo. Baadhi ya mashabiki walihoji iwapo alinyoa kweli au kama ilikuwa ni kiki ya mitandao. Katika sehemu ya maoni, baadhi ya mashabiki walitoa pongezi wakisema muonekano wake mpya unampendeza na unampa sura ya “umakini mpya”, huku wengine wakitilia shaka ukweli wa madai yake. “Bahati hata kama ni kiki, umetuburudisha. Ila tuambie ukweli – hizo rasta bado zipo ama?” aliandika mmoja wa mashabiki. Muimbaji huyo, anayejulikana kwa kubadili mitindo ya maisha hadharani, ameendelea kuvutia vichwa vya habari kwa sababu mbalimbali kuanzia maisha ya ndoa, siasa, hadi mitindo ya uvaaji. Sasa, inaonekana hata nywele zimeingia kwenye orodha ya vitu vinavyoleta mjadala. Hadi sasa, Bahati hajatoa kauli rasmi kuhusu video hiyo au kama kweli alinyoa, lakini haijazuia mashabiki wake kuendelea kutoa maoni mseto kati ya wanaomsifu na wanaohoji ukweli wa mabadiliko yake

Read More