Donjo Maber: Wimbo Mpya wa Iyanii na Dufla Wateka Mitandao kwa Midundo ya Afro-Dancehall

Donjo Maber: Wimbo Mpya wa Iyanii na Dufla Wateka Mitandao kwa Midundo ya Afro-Dancehall

Wimbo mpya “Donjo Maber” wa wasanii wa Kenya Iyanii na Dufla Diligon unaendelea kutikisa mitandao ya kijamii na kuchezwa sana kwenye vituo vya redio. Donjo Maber, ni msemo wa jamii ya Luo unaomaanisha jambo limeweza au limetiki, kwenye hii single umetumika kama kauli ya ushindi na vibe nzuri mitaani. Wimbo huu ambao ni moja kati ya single itakayopatikana kwenye Album mpya ijayo ya Iyanii, unachanganya midundo ya Afrobeat na dancehall kwa ustadi mkubwa. Vocals za Dufla zinabeba hisia za mitaani huku Iyanii akitamba na uchezaji wa maneno unaonata. Beat ni kali na mashairi ni mepesi, yanayokaririka kirahisi, jambo ambalo limeufanya kuwa maarufu mitandaoni hasa kupitia #DonjoMaberChallenge kwenye TikTok na Instagram. Video rasmi ni ya rangi kali, nguo za kuvutia na densi zilizopangwa kitaalam. Ingawa haina hadithi nzito, inalenga vibe ya kusherehekea, jambo linaloifanya kuwavutia sana vijana. Tayari ndani ya siku 10 imevuma YouTube ikiwa na zaidi ya views laki 3 huku ikishikilia nafasi ya 6 kwenye trending tab nchini Kenya. Kwa ujumla, Donjo Maber ni ushahidi kuwa muziki wa Kenya unaendelea kukua na kuchukua nafasi katika soko la Afrika na dunia. Ushirikiano kati ya Iyanii na Dufla umeleta ladha ya kipekee ambayo inakonga nyoyo za mashabiki. Ni wimbo wa kujivunia, wa kufurahia, na bila shaka, una nafasi kubwa kuwa hitsong ya mwaka.

Read More
 Dufla Amvamia Mulamwah Kwa Maneno Makali Mtandaoni

Dufla Amvamia Mulamwah Kwa Maneno Makali Mtandaoni

Msanii wa muziki wa dancehall nchini Kenya, Dufla Diligon, amemkemea hadharani mchekeshaji maarufu Mulamwah, akimtuhumu kwa vitisho na usumbufu wa simu. Kupitia ujumbe mkali aliouweka katika ukurasa wake wa mitandao ya kijamii, Dufla alieleza hasira zake na kuonyesha kutoridhishwa na tabia ya Mulamwah. “Mulamwah stop threatening me!! Mimi mahali nimezaliwa wewe hata hauwezi survive. Hizi vitisho punguza… ama unaona mimi sina sauti, I mean I don’t have bass?!! On a serious note, stop calling me na kunitishia, mimi ni warrior, am not a coward!!!!” Dufla aliandika Instagram. Ujumbe huo umeibua gumzo mitandaoni, huku mashabiki wa muziki na wafuasi wa burudani wakitaka kufahamu chanzo cha mvutano huo. Wengi wameunga mkono msimamo wa Dufla, wakisema kuwa watu maarufu wanapaswa kutumia ushawishi wao kwa njia ya kujenga, si ya kuharibu.  Siku chache kabla ya taarifa hiyo, Dufla alikuwa amedai kwamba Mulamwah alimblock kwenye Instagram bila sababu ya msingi. Katika ujumbe huo, Dufla alimshauri Mulamwah kuacha kuwa na “feelings” kupita kiasi na kuzingatia mambo ya maana. Mvutano kati ya wawili hao ulianza miaka michache iliyopita, kufuatia madai kuwa Dufla alikuwa anamnyemelea baby mama wa Mulamwah, Carol Sonnie, jambo ambalo lilizua taharuki kubwa kwenye mitandao ya kijamii wakati huo. Ingawa hakuna uthibitisho wa moja kwa moja kuhusu uhusiano kati ya Dufla na Sonnie, hali hiyo ilisababisha sintofahamu kubwa kati yao.

Read More
 Dufla Diligon Amlalamikia Mulamwah kwa Kumblock Instagram

Dufla Diligon Amlalamikia Mulamwah kwa Kumblock Instagram

Msanii wa muziki wa Kenya, Dufla Diligon, amezua mjadala mtandaoni baada ya kufichua kuwa amefungiwa (blocked) na mchekeshaji maarufu Mulamwah kwenye mtandao wa Instagram. Kupitia Instastory yake, Dufla alisimulia tukio hilo kwa mshangao na utani, akisema kuwa aligundua amefungiwa wakati alipokuwa akitafuta akaunti ya Mulamwah akiwa katika mazungumzo na msanii Lyanii.  “Jana tulikuwa na mazungumzo na @officialiyanii, halafu nikaamua kutafuta akaunti ya Mulamwah kwenye IG. Nilishangaa kuona nimefungiwa. Kumbe mimi na Obinna tuko kwa listi moja!” aliandika Dufla. Katika ujumbe wake, Dufla hakusita kuonyesha mshangao wake na hata kumtaka Mulamwah “kupunguza hisia”, akionekana kutofahamu chanzo cha hatua hiyo ya mchekeshaji huyo.  “Punguza feelings buda!!!” aliongeza, kwa mtindo wa utani lakini uliobeba ujumbe mzito. Hadi sasa, Mulamwah hajatoa majibu yoyote hadharani kuhusu hatua hiyo, wala kueleza sababu ya kuwazima Dufla na Obinna kwenye ukurasa wake wa Instagram. Hata hivyo, mashabiki wa pande zote wameendelea kutoa maoni tofauti, wengine wakisisitiza haja ya kuwepo kwa mawasiliano ya moja kwa moja kati ya wahusika badala ya kupeana block mitandaoni.

Read More
 Dufla Diligon aweka wazi jina la EP yake mpya

Dufla Diligon aweka wazi jina la EP yake mpya

Mwanamuziki wa Dancehall Dufla Diligon amelitaja jina la EP yake mpya anayotarajia kuiachia hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram amesema EP hiyo ameiita “Zone”, na ana mpango wa kuachia wimbo wa kwanza kutoka kwa EP hiyo ambayo ameitaja kuwa ni bonus track. “Mheshimiwa @jalangoo alilalamika sana kwamba sijatoa ngoma siku nyingi. This week we drop a bonus track off my incoming EP ‘ZONE’ Thank you to everyone who keep supporting me. Much love to you all 💪🏿❤️🙏🏿”, Aliandika. Hata hivyo, Dufla ambaye amekuwa akisuasua kimuziki bado hajaweka wazi ni lini EP hiyo itatoka rasmi na itakuwa na nyimbo ngapi. Ikumbukwe kuwa, huu unaenda kuwa ujio wa kwanza kwa Dufla Diligon kuachia tangu ajiondoe kwenye label ya muziki ya GrandPa records.

Read More
 Mrembo Arnelisa Muigai akata penzi la mwanamuziki Dufla Diligon

Mrembo Arnelisa Muigai akata penzi la mwanamuziki Dufla Diligon

Huenda juhudi za mwanamuziki Dufla Diligon zikagonga mwamba baada ya mrembo Arnelisa Muigai kukataa hadharani ombi la msanii huyo kutaka kuingia naye kwenye mahusiano ya kimapenzi. Kupitia ukurasa wake wa Instagtam Arnelisa amesikitishwa na kitendo cha Dufla kutumia sarakasi nyingi mtandaoni kwa ajili ya kuteka hisia zake huku akisema kuwa mapenzi hayalazimishwa. Kauli ya Arnelisa imekuja mara baada ya video kusambaa mtandaoni ikiwaonyesha wasanii KRG The Don na Arrow Boy kwenye moja ya night club wakimliwaza Dufla Diligon ambaye alikuwa analilia penzi la Arnelisa. Utakumbuka wiki kadhaa zilizopita Dufla alijitokeza wazi na kudai kuwa anatamani kuingia kwenye mahusiano na Arnelisa ambapo alienda mbali zaidi na kuachia wimbo wake uitwao Arnelisa uliokuwa ukisifia urembo wa Arnelisa. Hayo yamekuja baada ya Arnelisa kutangaza hadharani kukamilisha mchakato mzima wa kuvunja ndoa yake na mwanamuziki bongo fleva Ben Pol.

Read More
 DUFLA DILIGON ADOKEZA UJIO WA EP YAKE MPYA

DUFLA DILIGON ADOKEZA UJIO WA EP YAKE MPYA

Mwanamuziki wa dancehall nchini Dufla Diligon ametangaza ujio wa EP yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia ndani ya mwaka huu wa 2022. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Dufla amethibitisha ujio wa ep hiyo kwa kusema kwamba anaendelea na mchakato wa kuandaa ep mpya huku akiwataka mashabiki wake wakae mkao wa kula kuipokea EP yake hiyo. Hata hivyo hajeweka wazi Idadi ya ngoma wala tarehe rasmi ambayo EP yenyewe itaingia sokoni ila amedokeza ujio wa kolabo yake na Visita ambayo ataachia muda wowote kuanzia sasa. Hii inaenda kuwa EP ya kwanza kwa mtu mzima Dufla Diligon tangu aanze safari yake ya  muziki.

Read More
 DUFLA DILIGON AZUA GUMZO MTANDAONI, AKIRI KUWA BABA WA MTOTO WA CAROL SONIE

DUFLA DILIGON AZUA GUMZO MTANDAONI, AKIRI KUWA BABA WA MTOTO WA CAROL SONIE

Mwanamuziki wa Dancehall nchini Dufla Diligon ameingia kwenye headlines mara baada ya kukiri kuwa baba wa mtoto wa Carol Sonie ambaye ni mpenzi wa zamani mchekeshaji Mulamwah. Katika mahojiano na Mungai Eve, Dufla amesema aliumizwa na kitendo cha Mulamwah kumkana hadharani mtoto huyo huku akisema kwamba yupo tayari kutoa matunzo kwa mtoto wa Carol Sonie kwani wana ukaribu na mrembo huyo. “Namjua Caro na siwezi taka kuongelea mambo mob sahi kwa sababu Mulamwah amewaka sana na hiyo stori ni moto. Niliona Mulamwah alikataa mtoto lakini mimi siwezi kataa huyo mtoto naweza mchukua ni msaidie. Mi am ready kumchukua, kumsaidia na mama yake. Sonnie ni mabeshte .. ” Alisema Dufla Diligon ameweka wazi hayo mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa huenda msanii huyo ndiye baba ya mtoto wa Carol Sonie kutokana na picha yake na mrembo huyo kusambaa mitandaoni wiki kadhaa zilizopita.

Read More