Dulla Makabila Aonya Vijana Wanaodharau Wanawake Wavumilivu

Dulla Makabila Aonya Vijana Wanaodharau Wanawake Wavumilivu

Msanii wa Singeli, Dulla Makabila, ametoa ushauri mzito kwa vijana wenzake ambao bado hawajafanikwa kimaisha lakini wako kwenye mahusiano. Kupitia ujumbe wake Instagram, Dulla Makabila amesema kuwa iwapo kijana hana fedha kwa sasa na mwanamke wake anaonyesha uvumilivu na kuendelea kusimama naye, basi asiruhusu kumpoteza mwanamke huyo kwa sababu ya mapungufu madogo aliyo nayo. Msanii huyo, amefafanua kuwa katika safari ya maisha, ni vigumu sana kwa mtu aliyefanikiwa kifedha kugundua mwanamke anayempenda kwa dhati na yupi anayempenda kwa ajili ya pesa zake. Kwa mtazamo wa msanii huyo, mwanamke anayechagua kubaki na mwanaume katika kipindi kigumu cha maisha ni wa thamani kubwa, kwani anathibitisha mapenzi ya kweli na sio ya kimaslahi.

Read More
 Bahati akoshwa na wimbo wa Dullah Makabila, “Pita Huku”

Bahati akoshwa na wimbo wa Dullah Makabila, “Pita Huku”

Mwimbaji nyota wa muziki toka Kenya, Bahati ameonyesha kukoshwa na ubunifu alioutumia staa wa Singeli nchini, msanii Dulla Makabila kwenye video ya wimbo wake mpya Pita Huku ulioibua mijadala juu ya mengi kufuatia yaliyo zungumziwa kwenye wimbo huo. Akiacha koment kwenye video hiyo katika mtandao wa YouTube, ujumbe wa Bahati unasomeka, “Huu ni Ubunifu Kaka Yangu. Hongera kwa Muziki mzuri”. Mbali na Bahati pia na wengine wengi wameacha komenti zao wakiusifia ubunifu uliofanywa kwenye kazi hiyo. Wimbo wa “Pita Huku” ambao umetoka Jumatatu ya wiki hii umefanikiwa kupata mapokezi makubwa kutoka kwa wadau mbalimbali wa muziki pamoja na mashabiki kwa ujumla.

Read More