Eddie Butita Avunja Kiapo Cha Kutovalia Pyjama Inayofanana na Mpenzi Wake
Mchekeshaji kutoka Kenya Eddie Butita amejipata njia panda baada ya kushiriki picha pamoja na mpenzi wake Cele Terer wakiwa wamevalia Pyjamas mfanano ikiwa ni miaka miwili imepita tangu akashifu vikali kitendo hicho kama ushamba uliopitiza. Kupitia Instagram, Butita alichapisha misururu ya picha maridadi kwenye ukurasa wake wa Instagram akiwa na mpenzi wake Cele, wakiwa wamepiga pozi za kimahaba kando ya mti wa Krismasi uliopambwa. Wawili hao walionekana wakiwa na furaha tele, huku wote wakiwa wamevalia pyjamas za Krismasi zenye muundo mmoja. Furaha hiyo ya Butita ilidumu kwa muda mfupi kabla ya walimwengu wenye kumbukumbu kali kufufua kauli yake ya Disemba 25, mwaka 2025. Katika video hiyo iliyosambazwa sana, Butita alikiri mbele ya mashabiki wake kuwa hatowahi kamwe kuvalia mavazi yanayofanana na mpenzi wake kisha akapost mitandaoni. Butita alisema kitendo hicho ni ushamba ambapo alienda mbali zaidi akawataka mashabiki wamweka kwa maombi ili asije kuvunja kiapo chake na kukufuru alichokitamka. Kufufuka kwa video hiyo imeashiria wazi kwamba mchekeshaji huyo hatimaye amezidiwa na nguvu ya mahaba, na hivyo kujisalimisha kwenye mahitaji ya mpenzi wake Celest Terer. Wengi wamechukulia hili kama uthibitisho wa msemo kwamba mapenzi hayana kiapo, na kwamba hata watu wenye msimamo mkali wanaweza kubadilika wanapokuwa kwenye uhusiano.
Read More