Eddy Yaawe Afichua Sababu ya Kutooa Licha ya Kuwa na Watoto Kadhaa

Eddy Yaawe Afichua Sababu ya Kutooa Licha ya Kuwa na Watoto Kadhaa

Mwanamuziki na mwanasiasa wa Uganda, Eddy Yaawe, amesema bado hajawa tayari kuingia kwenye ndoa licha ya kuwa na watoto kadhaa kutoka kwa mahusiano tofauti. Akihojiwa na kituo cha televisheni nchini Uganda, Yaawe alieleza kuwa hajawahi kuhofia mahusiano ya kimapenzi, lakini anaamini ndoa ni hatua ya kudumu inayohitaji maandalizi ya kiakili na kihisia. Yaawe alisema kuwa haoni haja ya kuharakisha ndoa kwa sababu tayari ana watoto, wengi wao wakiwa vyuoni, na maisha yake hayaonyeshi upweke. Alisisitiza kuwa anasubiri kumpata mwenza wa kweli atakayekuwa tayari kushirikiana naye maisha ya kudumu, si kwa shinikizo la jamii au umaarufu.  “Sijawa tayari kwa ndoa; nina watoto, lakini siishi maisha ya upweke. Ndoa si kitu cha kuharakisha. Nataka kuingia kwenye ndoa nikiwa na mtu nitakayeishi naye milele. Nitaoa wakati nikiwa tayari,” alisema Yaawe. Kauli hiyo imezua maoni mseto kutoka kwa mashabiki na wadau wa burudani, baadhi wakimpongeza kwa uaminifu wake, huku wengine wakitaka aweke mfano kwa vijana kwa kuhalalisha mahusiano. Hata hivyo, Yaawe anaendelea kuwa miongoni mwa wasanii na wanasiasa wenye ushawishi mkubwa nchini Uganda.

Read More
 EDDY YAAWE AWAJIBU WALIMWENGU KUHUSU WIMBO WA NETEZE ALIOMSHIRIKISHA MARTHA MUKISA

EDDY YAAWE AWAJIBU WALIMWENGU KUHUSU WIMBO WA NETEZE ALIOMSHIRIKISHA MARTHA MUKISA

Mwimbaji mkongwe kutoka Uganda Eddy Yaawe amekanusha madai kwamba alitaka wimbo wa “Neteze” aliomshirikisha martha mukisa uwe kwenye Youtube channel yake ili afaidi na mirabaha ya wimbo huo. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Eddy Yaawe amepuzilia madai hayo kwa kusema kwamba hajawahi pata pesa zozote kutoka kwenye channel yake ya youtube na uvumi huo unaosambaa mtandaoni kwa sasa ni njia ya uongozi wa Martha Mukisa kumtangaza msanii wao. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Love Yo” ameshikilia kuwa uhusiano wake na Martha Mukisa ungali mzuri licha ya kutokuwa na maelewano mazuri katika pindi cha wiki chache zilizopita. Kauli ya Eddy Yaawe imekuja mara baada ya watumiaji wa mitandao ya kijamii nchini Uganda kudai kwamba msanii huyo alifuta collabo yake na Martha mukisa kwenye mtandao wa youtube kwa sababu alitaka anufaike na mirabaha ya wimbo huo mwenyewe.

Read More