Eddy Yawe afunguka kuwanyanyasa kimapenzi wasanii wa kike

Eddy Yawe afunguka kuwanyanyasa kimapenzi wasanii wa kike

Mwimbaji wa zamani wa bendi ya Afrigo Eddy Yawe ameamua kuvunja kimya chake kuhusu tuhuma za kuwanyanyasa kimapenzi wasanii wa kike. Katika mahojiano yake hivi karibu Yawe amesema tuhuma zote alizozushiwa mtandaoni hazina ukweli wowote kwani ilikuwa njia ya baadhi ya watu kumshusha kimuziki Msanii huyo kutoka nchini Uganda amenyosha maelezo kuhusu ugomvi wake na Msanii Carol Nantogo akisisitiza kuwa chanzo cha kukosana kwao ni hatua ya mrembo huyo kudhani kuwa ilikuwa lazima watumbuize pamoja wimbo wao “Tukiggale” kila sehemu anayopata mwaaliko. Lakini ameeleza kuwa walikuja wakatatua tofauti zao baada ya Nantogo kumuomba msamaha na sasa wana uhusiano mzuri kikazi. Hitmaker huyo “Love Yo” amezungumzia pia suala la kutokuwa na maelewano mazuri na msanii Martha Mukisa kwa kusema kuwa utofauti wao uliibuka kutokana na masuala ya hakimiliki wa wimbo wao “Neteze” na sio kumnyanyasa kingono kama ilivyoripotiwa mtandaoni kwani madai hayo yaliibuliwa na watesi wake. Hata hivyo kuhusu sakata la kumdhulumu kimapenzi msanii chipukizi Sheebah Sumayiyah Eddy Yawe amesema suala hilo linatatuliwa faraghani na hivi karibuni sheria itafuata mkondo wake.

Read More
 CINDY SANYU AMKINGIA KIFUA EDDY YAWE KWA TUHUMA ZA KINGONO

CINDY SANYU AMKINGIA KIFUA EDDY YAWE KWA TUHUMA ZA KINGONO

Rais wa chama cha wasanii nchini Uganda Cindy Sanyu amedai kuwa hana uwezo wa kumsaidia msanii chipukizi Sumaiya Sheebah ambaye alidai kuwa alinyanyaswa kijinsia na Eddy Yawe. Cindy amesema mrembo huyo ana ushahidi wowote wa kuonyesha alidhulumiwa kingono na Eddy Yawe kwa kuwa hana mkataba wa kufanya kazi na msanii, hivyo itakuwa vigumu kumsaidia kisheria. Hitmaker huyo wa “Local Man” ametoa changamoto kwa wasanii kuhakikisha wanakuwa na mikataba ya kufanya kazi na wasanii wenzao kama njia ya kuwasaidia kisheria wakati wa matatizo. Utakumbuka juzi kati msanii chipukizi Sumaiya Sheebah aliibua madai kuwa Eddy Yawe amekuwa akimuitisha rushwa ya ngono ili waweze kufanya kazi ya pamoja, shutuma ambazo bosi huyo wa Dream Studios alikanusha vikali kwa kusema kwamba madai ya mrembo huyo hayana ukweli wowote kwani ni njia ya kuichafua brand yake ya muziki.

Read More
 EDDY YAWE ATUHUMIWA KUMNYANYASA KINJISIA MSANII CHIPUKIZI UGANDA

EDDY YAWE ATUHUMIWA KUMNYANYASA KINJISIA MSANII CHIPUKIZI UGANDA

Msanii Eddy Yaawe ameingia kwenye headlines mtandaoni mara baada ya msanii mwenye asili ya Uganda anayeishi nchini Denmark kumkashifu kwa madai ya kuhujumu shughuli zake za muziki. Msanii huyo anayefahamika kwa jina la Sumaya Sheebah amefunguka na kudai kuwa Eddy Yawe aliuuza wimbo wake kwa mtu mwingine bila ridhaa yake alipokataa kumpa rushwa ya ngono. Mrembo huyo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa licha ya kukubali kulipia gharama zote za kuandaa na kutayarishaji video ya wimbo huo, Eddy Yawe aliamua kufanya kazi hiyo na msanii mwingine aitwaye TYBA. Sheebah amedai alikutana na bosi huyo wa Dream Studios mwaka wa 2017 huko Copenhagen ambako walitia sahihi mkataba wa kufanya kazi pamoja ila tangu kipindi hicho amekuwa akimpa ahadi za uongo Hata hivyo Eddy Yawe amesalia kimya kuhusu tuhuma hizo za kutaka kimnyanyasa kinjisia binti huyo.

Read More
 EDDY YAWE ACHOSHWA KUPATANISHA BOBI WINE NA WASANII WENZAKE

EDDY YAWE ACHOSHWA KUPATANISHA BOBI WINE NA WASANII WENZAKE

Mwanamuziki kutoka Uganda Eddy Yawe amekiri kuchoshwa na kitendo cha kuwa mstari wa mbele kutatua tofauti za Bobi Wine na wasanii wenzake kila mara wanapoingia kwenye ugomvi. Katika mahojiano yake hivi karibuni Eddy Yawe amesema kama mwananchi wa kawaida  ana majukumu mengine ya kufanya ikiwemo kushughulikia familia yake na kuendelea kusukuma muziki wake licha ya kuwa Bobi Wine ni mdogo wake Hitmaker huyo wa ngoma ya “Neteze” amesema amechoshwa kutatua ugomvi wa bobi wine na wasanii wenzake hivyo atasusia kupokea lalama kutoka baadhi ya wasanii ikizingatiwa kuwa ni watu wazima. Hata hivyo amehapa kumaliza ugomvi ulioibuka kati ya Bobi Wine  na Eddy Kenzo kabla kuacha kabisa masuala ya kuwa mtatuzi wa mdogo wake bobi wine na wasanii wenzake.

Read More
 EDDY YAWE NA CAROL NANTONGO WAMALIZA TOFAUTI ZAO

EDDY YAWE NA CAROL NANTONGO WAMALIZA TOFAUTI ZAO

Carol Nantongo and msanii mkongwe nchini Uganda Eddy Yawe walitubariki na smash hit yao iitwayo “Tukigale” mwaka wa 2018. Wimbo huo ulifanya vizuri sokoni lakini wawili hao walikuja wakaiingia kwenye ugomvi kutokana na umiliki wake wa Tukigale kiasi cha kutotumbuiza wimbo huo kwenye matamasha mbali mbali ya muziki. Hata hivyo wikiendi hii iliyopita wawili hao walikutana jukwaani na wakatumbuiza pamoja wimbo wa Tukigale kwenye hafla moja ya harusi ambayo walialikwa kutoa burudani. Eddy Yawe na Carol Nantongo walionekana wakikumbatiana jukwaani kabla ya kuwaambia mashabiki zao kuwa wameweka tofauti zao kando kuhusu umiliki wa wimbo huo. Utakumbuka juzi kati Eddy Yawe walizozana na msanii mwenzake Martha mukisa baada ya kuachia kolabo yao itwayo Neteze.

Read More
 EDDY YAWE APINGA VIKALI KUMDHULUMU KIMAPENZI MARTHA MUKISA

EDDY YAWE APINGA VIKALI KUMDHULUMU KIMAPENZI MARTHA MUKISA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Eddy Yawe amekanusha madai ya kumnyanyasa kimapenzi msanii wa kike nchini humo Martha Mukisa. Katika mahojiano yake hivi karibuni Yawe amesema madai hayo hayana ukweli wowote huku akisisitiza kwamba uhusiano wake na Martha Mukisa ulikuwa wa kikazi tu. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Love Yo” amesema walitafautiana kimawazo na Martha Mukisa wakati uongozi wake ulitaka kuchukua wimbo wake Neteze kwa nguvu bila ridhaa yake kwa kumnyima haki za umiliki wa wimbo huo walipopakia kwenye akaunti ya Youtube ya mrembo huyo. Kauli ya Eddy Yawe imekuja mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kuhoji kuwa ugomvi kati yake na Martha Mukisa kuhusu umiliki wa wimbo wa Neteza ulitokana na mrembo huyo kukataa kutoka nae kimapenzi.

Read More
 EDDY YAWE NA MARTHA MUKISA WAINGIA KWENYE UGOMVI KISA UMILIKI WA WIMBO WA “NETEZE”

EDDY YAWE NA MARTHA MUKISA WAINGIA KWENYE UGOMVI KISA UMILIKI WA WIMBO WA “NETEZE”

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Eddy Yawe ameingia kwenye ugomvi na msanii chipukizi nchini humo Martha Mukisa kuhusu umiliki wa wimbo wao uitwao “Neteze”. Hii ni baada ya Eddy Yawe kufuta wimbo huo kwenye akaunti ya youtube ya msanii Martha Mukisa kwa kigezo kuwa wimbo wa “Neteze” ni wake. Kulingana na Eddy Yawe yeye ni ndio mmiliki halisi wa wimbo huo kwani aligharamia pesa zote za kutayarisha audio pamoja na video Hata hivyo chanzo cha karibu na Martha Mukisa kinadai kuwa msanii hyuo anaamini kwamba atarejesha wimbo kwenye akaunti yake ya youtube wakati huu uongozi upo kwenye mazungumzo na Eddy Yawe kutafuta suluhu ya mgogoro ulioibuka katika yao. Utakumbuka kipindi cha nyuma Eddy Yawe walizozana na Carol Nantogo kuhusu umiliki wa wimbo wao uitwao Tukigale ambapo aliweza kumpokonya mrembo huyo hakimiliki zote za wimbo huo.

Read More
 EDDY YAWE AJUTIA KUJIUNGA NA SIASA, AKIRI KUPOTEZA PESA NYINGI

EDDY YAWE AJUTIA KUJIUNGA NA SIASA, AKIRI KUPOTEZA PESA NYINGI

Msanii mkongwe kwenye muziki nchini Uganda Eddy Yawe amekiri kujutia uamuzi wake wa kujiunga na siasa. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Eddy Yawe amesema hajafaidi kivyovyote na siasa licha ya kuwekeza pesa nyingi kwenye azma yake kuwa meya wa manispaa ya Kira nchini Uganda. Ikumbukwe Eddy Yawe kwenye mahojiano yake mbali mbali amekiri kuwa aliuza mali yake nyingi kwa ajili ya kufadhili kampeini zake za kisiasa kitu ambacho amekuwa akijutia kwani amepoteza pesa nyingi. Eddy Yawe kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2021 nchini alijaribu kumuondoa mamlakani meya wa sasa wa Manispaa ya Kira nchini Uganda lakini hakufanikiwa kumng’atua afisini.

Read More
 EDDY YAWE AMTAKA CATHERINE KUSASIRA KUJIUNGA NA CHAMA CHA KISIASA CHA NUP

EDDY YAWE AMTAKA CATHERINE KUSASIRA KUJIUNGA NA CHAMA CHA KISIASA CHA NUP

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Eddy Yawe ametoa wito kwa msanii mwenzake Catherine Kusasira kujiunga na chama cha NUP kinachongozwa na Bob Wine. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Eddy Yawe amesema kama kweli Kusasira amechoshwa na chama tawala cha NRM,itakuwa ni jambo la busara kwa msanii huyo kujiunga na NUP, chama ambacho kinapigania demokrasia nchini Uganda. Kauli ya Eddy Yawe imekuja mara baada ya Catherine Kusasira kukiri hadharani kuwa Chama cha NRm kimemtelekeza licha ya kuingia kifua kwenye uchaguzi mkuu wa mwaka wa 2021,  hivyo anafikiria kujiondoa kwenye chama hicho. Utakumbuka mwaka wa 2021 Catherine Kusasira alimkashifu Bob Wine hadharani kwa hatua ya kushindana na  Rais Yoweri Museveni kwenye uchaguzi mkuu uliopita nchini Uganda.

Read More
 EDDY YAWE AWAPA SOMO WASANII WA UGANDA

EDDY YAWE AWAPA SOMO WASANII WA UGANDA

Mkongwe wa muziki kutoka nchini uganda Eddy yawe ametoa changamoto kwa wasanii kutia bidii kwenye kazi zao za muziki ili waweze kutimiza malengo yao maishani. Yawe ambaye ni kaka wa bobi wine amesema kiwanda cha muziki nchini uganda kina fedha nyingi hivyo wasanii wanapaswa kujenga tabia ya kuweka akiba badala ya kutumia pesa zao zote kwenye starehe.. Kauli ya Eddy yawe imekuja mara baada ya kukamilisha ujenzi wa mjengo wake wa kifahari uliomgharimu takriban shillingi millioni 155 viungani mwa jiji la kampala. Licha ya Eddy Yawe kusisitiza kwamba ni bidii yake ndio imechangia kukamilisha mjengo wake wa kifahari baadhi ya watumiaji wa mitandao ya kijamii wanahoji kwamba mradi wake huo ulifadhiliwa na serikali.

Read More