Mwanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya akiri kuua kisa usaliti

Mwanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja nchini Kenya akiri kuua kisa usaliti

Mwanaharakati wa mapenzi ya jinsia moja (LGBTG) Nchini Jackson Odhiambo amekiri kumuua mpenzi na mume wake Edwin Chiloba kwa madai ya kumsaliti kimapenzi. Wawili hao walikuwa wanaishi pamoja kama mke na mme kwa takribani mwaka mmoja kabla ya tukio hilo la kutisha. Odhiambo almaarufu Lizer ambaye alikiri kuwa alilazimika kupanga mauaji hayo kwa usaidizi wa marafiki wengine wawili baada ya kugundua kuwa mpenzi Edwin Chiloba alikuwa na mahusiano na mwanamume mwingine. Inasemekana Lizer alitumia simu ya mpenzi wake kumtahadharisha mlinzi kuwa wanahama eneo hilo, baadaye aliondoka na vitu vilivyowekwa kwenye sanduku la chuma bila kujua ni mwili wa Edwin ambao ulipatikana umbali wa kilomita 20 kutoka eneo la tukio.

Read More
 Mwanamitindo akutwa amefariki Kenya

Mwanamitindo akutwa amefariki Kenya

Polisi katika kaunti ya Uasin Gishu wanachunguza chanzo cha mauaji baada ya mwili wa mwanamitindo maarufu Edwin Chiloba kukutwa umetupwa ukiwa ndani ya sanduku la chuma. Kulingana na chanzo kimoja cha habari ,mwendesha Bodaboda aliona gari ambalo halikuwa na namba likitupa sanduku la chuma kando ya barabara ya Kipenyo – Kaptinga. Kisa hicho kiliripotiwa kwa polisi wa Uasin Gishu ambao walifika eneo la tukio na walipofungua sanduku hilo, walikuta mwili wa mwanamume aliyekuwa amevalia nguo za kike uliokuwa ukianza ukioza. Baadaye ilibainika kuwa marehemu alikuwa mbunifu wa mitindo wa Eldoret Edwin Chiloba. Mwili huo ulipelekwa katika hospitali ya rufaa ya Moi ukisubiri uchunguzi wa maiti kubaini chanzo cha kifo hicho.

Read More