EKO DYDDA AWAPA SOMO VIJANA KUELEKEA UCHAGUZI MKUU WA AGOSTI 9
Wakati joto la uchaguzi mkuu likizidi kupanda katika maeneo mengi nchini,mwanamuziki aliyegeukia siasa Eko Dydda amewataka vijana kuwa makini na viongozi wanaotoa rushwa, kwa ajili ya kuwashawishi kuchagua upya kwenye uchaguzi wa Agosti 9. Katika mahojiano na mpasho Eko Dydda ametoa changamoto kwa vijana kuwa na dhamira ya dhati kuwakataa wagombea watakaojaribu kuiendekeza rushwa wakati huu wa kampeini kwani ni njia ya kuwapofusha macho na matokeo yake ni taifa kupata viongozi wasiofaa. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Vidole” amekiri kwamba upungufu wa uadilifu miongoni mwa watu wengi nchini unatokana na tatizo la rushwa ambalo pia ni miongoni mwa changamoto kubwa dhidi ya amani, utulivu na mshikamano. Hata hivyo amewahimiza wakenya kutowachagua viongozi kwa misingi ya vyama vya kisiasa na badala yake kuwachagua viongozi wenye maono ya maendeleo na watakaojali maslahi yao. Utakumbuka Eko Dydda anawania wadhfa wa uwakilishi wadi ya Mathare kaskazini kwenye uchaguzi mkuu ujao kama mgombea uhuru.
Read More