Roboti wa Tesla “Optimus” Aonyesha Uwezo wa Kushangaza Katika Kucheza Muziki Kama Mwanadamu

Roboti wa Tesla “Optimus” Aonyesha Uwezo wa Kushangaza Katika Kucheza Muziki Kama Mwanadamu

Katika hatua nyingine ya kuvutia katika maendeleo ya teknolojia ya roboti, Bilionea Elon Musk ametoa onyesho jipya la roboti wa kampuni ya Tesla, anayejulikana kama Optimus. Kupitia video iliyosambazwa mitandaoni, roboti huyo ameonekana akicheza aina mbalimbali za muziki kwa ustadi wa kushangaza, akionyesha uwezo wa kufanya dance moves zinazofanana na za mwanadamu wa kawaida. Roboti huyo, ambaye awali alizinduliwa kama sehemu ya ndoto ya Tesla kuunda roboti wa kusaidia kazi mbalimbali, sasa amepewa uwezo wa kutambua sauti, kuchanganua midundo ya muziki, na kuratibu harakati zake kwa ufanisi wa hali ya juu. Katika video hiyo, Optimus anaonekana akijibu mabadiliko ya midundo ya muziki kwa hatua sahihi, jambo linalodhihirisha maendeleo makubwa katika mfumo wa AI (Artificial Intelligence) unaomwendesha. Kwa mujibu wa Musk, uwezo huu wa Optimus kucheza muziki si burudani tu, bali pia ni sehemu ya majaribio ya kufanya roboti huyo aweze kuelewa mazingira yake vizuri zaidi kupitia mchanganyiko wa sauti, mwonekano, na mwendo. Hii inaashiria kuwa Tesla inalenga zaidi kazi za kawaida kama kubeba mizigo au kusaidia nyumbani na ujio wa  rboti hiyo inalenga kurahisisha zaidi kazi za binadamu Hatua hii mpya inachochea mjadala mpana kuhusu mustakabali wa roboti katika maisha ya kila siku, huku wengine wakijiuliza ni lini tutaweza kuwa na wasaidizi wa nyumbani wanaojua hata kucheza nasi.

Read More
 Twitter kufanya mabadiliko tena

Twitter kufanya mabadiliko tena

Mkurugenzi Mtendaji Mkuu wa mtandao wa Twitter, Elon Musk ametangaza kwamba, Twitter inatarajia kuongeza kipengele kipya ndani ya jukwaa hilo kitakacho onesha idadi ya watu waliopita na kuona chapisho (tweet) la mtumiaji. Musk ambaye tangu aununue mtandao huo Oktoba mwaka huu kwa dola bilioni 44, kasi yake ya kuweka vipengele vipya katika jukwaa hilo inakosolewa vikali. Kipengele hicho, ambacho tayari kipo kwa ajili ya video, kitaonyesha nii kiasi gani Twitter iko hai kuliko inavyoweza kuonekana,” Musk aliandika, akifafanua kwamba “Zaidi ya asilimia 90 ya watumiaji wa Twitter wanasoma, lakini hawa- tweet, kujibu au kuonesha hisia (like) kama matendo ambayo yako wazi.”

Read More
 Elon Musk kufanya majaribio ya kifaa cha kuwezesha ubongo wa binadamu kuwasiliana na kompyuta.

Elon Musk kufanya majaribio ya kifaa cha kuwezesha ubongo wa binadamu kuwasiliana na kompyuta.

Bilionea wa teknolojia Elon Musk amesemaleo kwamba moja ya kampuni zake itaweza katika miezi sita kuwa na uwezo wa kupandikiza kifaa kwenye ubongo wa mwanadamu kitakachoruhusu mawasiliano na kompyuta. Kifaa hicho kilichotolewa na kampuni ya Neuralink ya Musk, kitaruhusu mtumiaji kuwasiliana moja kwa moja na kompyuta kupitia mawazo yao, alisema. “Tumewasilisha nadhani karatasi zetu nyingi kwa FDA (Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani) na tunafikiri pengine katika muda wa miezi sita tunapaswa kuwa na Neuralink yetu ya kwanza katika binadamu.” alisema katika wasilisho la kampuni. “Tumekuwa tukifanya kazi kwa bidii ili kuwa tayari kwa mwanadamu wetu wa kwanza mwenye kipandikizi hiki (implant), na ni wazi tunataka kuwa waangalifu sana na hakika kwamba itafanya kazi vizuri kabla ya kuweka kifaa ndani ya mwanadamu.” alisema Musk.

Read More
 Elon Musk anadai Apple imetishia kuiondoa Twitter

Elon Musk anadai Apple imetishia kuiondoa Twitter

Tajiri namba moja duniani na mmiliki wa mtandao wa Twitter, Elon Musk ameeleza kwamba Kampuni ya Apple inatishia kuizuia Twitter kupatikana kwenye App Store. Musk ambaye aliinunua Twitter kwa zaidi ya KSh. Trilioni 5, amesema Apple hawajatoa sababu za kwanini wanataka kufikia uamuzi huo. Wiki iliyopita Elon Musk alidokeza kwamba kama Apple watachukua maamuzi hayo ya kuifungia Twitter, basi itakuwa nafasi nzuri ya kuleta simu zake mwenyewe.

Read More