Elsa Majimbo Azua Mjadala Mtandaoni kwa Kauli Kuhusu Urembo Wake

Elsa Majimbo Azua Mjadala Mtandaoni kwa Kauli Kuhusu Urembo Wake

Mchekeshaji na mshawishi maarufu wa mtandaoni, Elsa Majimbo, amefichua hisia zake kuhusu maoni anayopewa mara kwa mara kuhusu urembo wake, akisema wakati mwingine anahisi kama watu wanamtania. Kupitia video aliyochapisha kwenye Instagram, Majimbo alisema kuwa sifa nyingi anazopokea kuhusu urembo wake huwa zinamchanganya, kwani ni nyingi kiasi kwamba zinaanza kuonekana kama mzaha. “Kitu cha kwanza ambacho watu husema kila wanaponiona ni jinsi nilivyo mrembo hadi nafikia kuhisi kama wananitania,” alisema Majimbo kwa sauti ya dhihaka iliyoambatana na tabasamu. Kauli hiyo imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakieleza kuwa ni kawaida kwa watu maarufu kupokea sifa nyingi, huku wengine wakisema ni muhimu kwa watu kuelewa athari ya sifa za kupindukia kwa mtu binafsi. Elsa Majimbo, ambaye amejizolea umaarufu kimataifa kupitia ucheshi wake wa kipekee na mtindo wa kujiamini, amekuwa mfano kwa vijana wengi barani Afrika. Hata hivyo, kauli yake inaonyesha kuwa hata watu maarufu hukumbana na changamoto za kihisia kuhusu namna wanavyotazamwa na jamii.

Read More