Eminem ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Hiphop – 50 Cent

Eminem ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Hiphop – 50 Cent

Rapa 50 Cent hakubaliani na hoja isemayo kwamba Jay-Z ana mchango mkubwa kwenye muziki wa Hip Hop kuliko Eminem. 50 Cent ameipinga hoja hiyo ambayo imesemwa na nyota wa zamani wa NBA, Jamal Crawford kwenye podcast ya Shaquille O’Neal, 50 Cent alishuka kwenye comment na kusema ni upuuzi mtupu. Sio mara ya kwanza kwa 50 Cent kumkingia kifua Eminem hasa pale inapokuja mijadala mizito ya muziki wa Hiphop, itakumbukwa Oktoba 2022 kwenye mahojiano na Ebro in The Morning, 50 Cent alisema “Rap God” Eminem hapewi heshima ambayo anastahili.

Read More
 50 cent adai Eminem hapewi heshima anayostahili

50 cent adai Eminem hapewi heshima anayostahili

Rapa mkongwe kutoka nchini Marekani 50 Cent amesema rapa Eminem hapewi heshima ya kutosha. Kwenye mahojiano yake na ‘Ebro In The Morning’ wakati akiitangaza series yake mpya (Hip Hop Homicides), 50 Cent amesema kwa mchango ambao Eminem ameuweka kwenye huu muziki wa Hiphop, anafikiri anastahili heshima zaidi ya ambayo anapewa kwa sasa. Ikumbukwe ‘Eminem’ ndiye rapa mwenye rekodi nyingi za mauzo yaani Most Certified Artist katika historia ya muziki nchini Marekani, mpaka sasa ana jumla ya certificate Million 73.5 kwa upande wa Gold & Platinums. Eminem anashikilia rekodi ya msanii aliyeuza singo nyingi zaidi katika kiwango cha (Gold) na (Platinum) yaani mauzo kuanzia nakala laki tano hadi milioni moja, akishika namba moja katika historia ya RIAA Awards.

Read More