Mbosso Aachia EP Mpya Room Number 3

Mbosso Aachia EP Mpya Room Number 3

Staa wa Bongo Fleva Mbosso ameanza ukurasa mpya katika muziki wake kwa kuachia EP yake ya tatu iitwayo Room Number 3, miezi michache baada ya kuondoka kwenye lebo ya WCB Wasafi. EP hiyo, ambayo ina nyimbo 7 bila collabo yoyote, tayari imechukua nafasi ya kwanza kwenye majukwaa makubwa ya muziki kama Apple Music na Spotify, hatua inayothibitisha kuwa Mbosso bado ni nguvu kubwa kwenye tasnia ya muziki wa Afrika Mashariki. Nyimbo zilizopo kwenye EP hiyo ni: Pawa, Nusu Saa, Tena, Merijaah, Siko Single, Aviola, na Asumani. Maudhui ya EP yanahusu mapenzi, maisha na hisia za kina, yakionyesha ubunifu wa Mbosso akiwa msanii huru. Kwa mashabiki wa muziki wa Kiswahili, Room Number 3 ni ishara ya mwanzo mpya kwa Mbosso, na sasa inapatikana kwenye majukwaa yote ya kidijitali.

Read More
 Jux Atoa EP Maalum Kuelezea Safari Yake ya Mapenzi na Mkewe Priscy

Jux Atoa EP Maalum Kuelezea Safari Yake ya Mapenzi na Mkewe Priscy

Msanii nyota wa Bongo Fleva, Juma Jux, ameachia rasmi kazi yake mpya ya muziki, EP iitwayo “A Day To Remember”, kama kumbukizi maalum ya ndoa yake na mkewe mpendwa, Priscy. Kupitia mitandao ya kijamii, Jux ameeleza kuwa mradi huu si kazi ya kawaida, bali ni simulizi ya maisha yao ya upendo, kuanzia mwanzo wa safari yao ya mahaba hadi furaha waliyonayo sasa kama wanandoa. EP hiyo imejaa hisia, utamaduni na usanii wa hali ya juu, ikiwa imeshirikisha mastaa wawili wakubwa: Phyno kutoka Nigeria na D Voice kutoka Tanzania. Jux ameamua kuunganisha ladha ya Afrika Mashariki na Magharibi ili kuwasilisha ujumbe wa upendo unaovuka mipaka ya lugha na mataifa. Kati ya watayarishaji walioweka mikono yao kwenye kazi hii ni S2kizzy, Foxx Made It, na Aykbeats, huku kazi ya mixing na mastering ikifanywa na Lizer Classic, jina kubwa katika ubora wa sauti Afrika. Katika ujumbe wake, Jux hakusita kumshukuru mkewe Priscy kwa kuwa chanzo cha msukumo wa EP hii, pamoja na familia yake, timu nzima ya wasanii na wahusika waliounga mkono kazi hiyo, na mashabiki waliomfuatilia kwa miaka mingi. Amesisitiza kuwa baada ya harusi yao rasmi, atatoa wimbo wa kipekee kama zawadi ya kufunga sura hii mpya ya maisha. EP “A Day To Remember” itapatikana kuanzia usiku wa leo kwenye majukwaa yote ya kidijitali ya kusikiliza muziki. Mashabiki tayari wameonyesha hamasa kubwa, wakisubiri kwa shauku kusikia mchanganyiko wa upendo na sanaa katika kazi hii ya kipekee.

Read More
 HANSTONE AACHIA RASMI THE AMAZING EP

HANSTONE AACHIA RASMI THE AMAZING EP

Msanii wa muziki wa kizazi kipya  nchini Tanzania Hassan Ramadhani Masanja maarufu kama ‘Hanstone’ ameachia EP yake mpya aliyoipa jina “The Amaizing” yenye jumla ya nyimbo 7. Mkali huyo ambaye alikuwa akihusishwa kuwa ni msanii mpya ajae kutoka lebo ya WCB, ameachia EP hiyo nje ya WCB. “The Amaizing EP” tayari inapatikana kwenye mitandao mbalimbali ya ku-stream muziki duniani. Hanstone ni mtoto wa pekee wa marehemu Banza Stone, alijipatia umaarufu kupitia ngoma ya Iokote aliyoshirikishwa na Maua Sama mwaka wa 2018.    

Read More