PROFESSOR JAY ATANGAZA UJIO WA EP MPYA
Staa mkongwe wa muziki wa rap nchini Tanzania, Professor Jay ameweka wazi kuachia EP mpya yenye jumla ya ngoma 5 hivi karibuni. Kupitia ukurasa wake wa instagram Professa Jay ameandika ujumbe unaosomeka “Badala ya kuwapa chakula cha ubongo kwa single moja naona kama niwape chakula cha EP ya nyimbo 5 au mnasemaje Maboss wangu” Professa Jay amebainisha hilo ikiwa ni takribani miezi 6 imepita tangu alipoachia hitsong yake iitwayo “Utanambia Nini”.
Read More