Msanii Mkongwe Eric Wainaina Amuunga Mkono Boniface Mwangi Kufuatia Kesi ya Uchochezi

Msanii Mkongwe Eric Wainaina Amuunga Mkono Boniface Mwangi Kufuatia Kesi ya Uchochezi

Mwanamuziki mkongwe nchini Kenya, Eric Wainaina, ametangaza hadharani kumuunga mkono mwanaharakati Boniface Mwangi, anayekabiliwa na mashtaka mazito kuhusiana na maandamano ya kupinga serikali yaliyofanyika Juni 25 mwaka 2025. Kupitia ujumbe kwenye mitandao ya kijamii, Wainaina aamempongeza Mwangi kwa ujasiri wake katika kupigania haki na kusema kuwa haki na uhuru wa kuandamana haupaswi kuchukuliwa kama ugaidi. Mkali huyo wa ngoma ya “Kitu Kidogo” amesisitiza kuwa Mwangi ni sauti muhimu katika taifa, akimtaja kama mzalendo anayestahili kuungwa mkono, na si kushinikizwa na vyombo vya usalama. “Boniface Mwangi ni rafiki na mpigania haki. Kumpigia vita ni kuwakandamiza Wakenya wote wanaotamani maisha bora. Tunasimama naye katika wakati huu mgumu,” alisema Wainaina Eric Wainaina ni mmoja wa wasanii wa Kenya waliokuwa mstari wa mbele miaka ya nyuma katika kuibua mijadala kuhusu haki, demokrasia na utawala bora kupitia muziki wake, na hatua yake imezidisha msukumo wa kuungwa mkono kwa Mwangi na wengine wanaopigania mabadiliko. Ikumbukwe Mahakama leo ilimwachilia Mwangi kwa dhamana ya shilingi milioni moja huku kesi yake ikipangiwa kutajwa tena tarehe 19 Agosti, 2025. Mwangi alizuiliwa katika Kituo cha Polisi cha Pangani kwa muda wa siku mbili kabla ya kufikishwa mahakamani siku ya Jumatatu, Julai 21, ambapo alikana mashtaka ya kumiliki silaha kinyume cha sheria.

Read More