Eric Omondi atangaza hali ya hatari kwa wasanii wanaopinga mswada wa kufufua muziki wa Kenya

Eric Omondi atangaza hali ya hatari kwa wasanii wanaopinga mswada wa kufufua muziki wa Kenya

Mchekeshaji Eric Omondi ana imani mswada wake wa kutaka muziki wa kenya kuchezwa kwa asilimia 75 kwenye vyombo vya habari utaidhinishwa kuwa sheria na Rais Willliam Ruto. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Omondi amesema alimaliza sehemu iliyokuwa inampa ngumu wa kuendelea na mswada huo huku akidai kilichobaki kwa sasa ni kuwashinikiza viongozi vijana walio kwenye bunge la 13 kupitisha ili wasanii waanze kupata riziki kupitia sanaa yao. Eric Omondi ambaye kwa muda mrefu amekuwa akipigana kwa udi na uvumba kutetea muziki wa Kenya, amesema atahakikisha wasanii wanaopinga mswada huo hawafaidiki na mafanikio yake pindi itakapoidhinishwa kuwa sheria kwani wengi wao wana ubinafsi wakujitakia makuu

Read More