Otile Brown Aumizwa na Habari za Ndoa ya Nabayet, Aandika Ujumbe wa Hisia Kali
Mwanamuziki wa Bongo R&B kutoka Kenya, Otile Brown, ameibua hisia mtandaoni baada ya kuonyesha maumivu na mshangao kufuatia habari za aliyekuwa mpenzi wake, Nabayet kutoka Ethiopia, kufunga ndoa. Kupitia Insta Story yake, Otile alionekana kushindwa kuficha hisia zake, hasa kwa kuwa alimtaja Nabayet katika wimbo wake mpya unaotarajiwa kuachiwa. Ameandika: “How does she go & get married after mentioning her on my new song dropping tomorrow… now I feel dueh…”, Otile aliandika hisia nyingi Maneno hayo yameibua hisia mseto mitandaoni, huku mashabiki wake wakimfariji na wengine wakihisi kwamba bado ana hisia kwa mrembo huyo. Uhusiano wa Otile Brown na Nabayet ulikuwa wa muda mrefu na wa hadharani, uliovutia mashabiki wengi kutoka Afrika Mashariki na Ethiopia. Wawili hao walionekana kuwa na mahusiano yenye upendo mkubwa kabla ya kuachana kimya kimya miaka michache iliyopita. Kabla ya habari za ndoa ya Nabayet, Otile alikuwa ameonekana kuendelea na maisha, lakini ujumbe huu mpya unaonyesha pengine bado kuna hisia zilizobaki. Mashabiki sasa wanasubiri kwa hamu wimbo mpya wa Otile Brown ili kusikia alivyomzungumzia Nabayet, huku wengi wakijiuliza kama hii itaathiri maudhui au hisia za kazi hiyo.
Read More