Eve Mungai Aumizwa na Taarifa za Mrembo wa Ex Wake Trevor Kupata Uja Uzito
Youtuber maarufu mtandaoni, Eve Mungai, ameonekana kuumizwa na taarifa za mpenzi wake wa zamani, Director Trevor, kuthibitisha kuwa anatarajia mtoto na mrembo wake wa sasa anayejulikana kama Kiki Love. Eve, kupitia mitandao yake, aliandika ujumbe ulioonekana kuashiria kwamba hana furaha kubwa na taarifa hiyo, akisema kuwa โsio wa kwanza kupata uja uzito.โ Kauli hiyo imeibua tafsiri tofauti kwa mashabiki wake, wengi wakihisi kwamba inaweza kuwa ishara ya machungu au hisia za wivu kwa hatua ya maisha ya ex wake licha ya kujaribu kujionyesha mwenye nguvu mbele ya umma. Hii inajiri baada ya Trevor mwenyewe kuthibitisha habari za ujauzito wa mrembo wake kupitia mitandao ya kijamii, akishare picha na ujumbe wa furaha akitangaza kuwa yeye na Kiki wanatarajia mtoto wao wa kwanza. Alienda mbali zaidi na kuwataka wafuasi wake wampendekezee majina watakayompa mtoto wao.
Read More