TYGA AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KUHUSU SAKATA LA KUMPIGA EX WAKE

TYGA AFUNGUKA KWA MARA YA KWANZA KUHUSU SAKATA LA KUMPIGA EX WAKE

Rapa kutoka nchini Marekani Tyga amefunguka kuhusu taarifa za kufunguliwa mashtaka kwa madai ya kumpiga ex wake Camaryn Swanson, Jumatatu wiki iliyopita. Tyga alijisalimisha kwenye mikono ya polisi mjini Los Angeles Jumanne  wiki iliyopita ambapo Tovuti ya TMZ ilidai kwamba tayari amefunguliwa mashtaka ya unyanyasaji wa nyumbani. Sasa baada ya kimya cha muda mfupi, Tyga ameamua kuweka wazi sakata hilo. Kupitia ukurasa wake wa instagram rapa huyo amekanusha kwa kusema madai hayo hayana ukweli wowote, kwani hakukamatwa na polisi na wala hakufunguliwa mashtaka yoyote bali alifika kituo hapo kujieleza. Kwa mujibu wa nyaraka za polisi wa Los Angeles, zinaonesha Michael Stevenson maarufu Tyga alishtakiwa kwa makosa ya uhalifu mnamo Oktoba 12 mwaka huu na aliachiwa masaa machache baadaye kwa dhamana ya shillingi millioni 5.5 za kenya.

Read More