EXRAY KUTUMBUIZA KWENYE HHAFLA YA KUAPISHWA KWA RAIS MTEULE WILLIAM RUTO

EXRAY KUTUMBUIZA KWENYE HHAFLA YA KUAPISHWA KWA RAIS MTEULE WILLIAM RUTO

Msanii Exray Taniua ametajwa kutumbuiza kwenye hafla ya kuapishwa kwa rais mteule William Ruto Jumanne juma lijalo. Mapema wiki hii hitmaker huyo wa “Sipangwingwi” aliposti video akiwa anakutana na rais huyo mteule na kisha kumpongeza kwa kuhifadhi ushindi wake baada ya mahakama ya juu kutupilia mbali kesi ya kupinga matokeo ya urais iliyowasilishwa na Azimio la Umoja. Exray atakuwa kwenye jukwaa moja na Guardian Angel, Solomon Mkubwa na wasanii wengine wengi ambao watatoa burudani kwenye hafla ya kuapishwa kwa rais William Ruto ambayo itahudhuriwa na marais wa mataifa mbali mbali. Guardian Angel na mke wake Esther Musila wameposti pia video wakiwa kwenye matayarisho katika uga wa Kimataifa wa Kasarani ambako hafla hiyo itafanyika.

Read More
 VDJ JONES AITAKA UDA KUMLIPA EXRAY KWA KUTUMIA WIMBO WAKE “SIPANGWINGWI” KWENYE KAMPEINI ZA KISIASA

VDJ JONES AITAKA UDA KUMLIPA EXRAY KWA KUTUMIA WIMBO WAKE “SIPANGWINGWI” KWENYE KAMPEINI ZA KISIASA

Dj maarufu nchini Vdj Jones ametoa wito kwa chama cha uda kinachoongozwa na Naibu Rais Dakta. William Ruto kumlipa msanii Exray kwa kutumia wimbo wake wa “Sipangwingwi” kwenye kampeni zao za kisiasa. Kwenye mahojiano na Plug tv, Vdj Jones ambaye pia mwanamuziki amesema ameumizwa sana na kitendo cha wanasiasa kutumia wimbo wa sipangwingwi kujitakia makuu ilhali Exray anaishi maisha ya uchochole mtaani. Hata hivyo ametaka haki itendeke juu ya suala hilo ila walimwengu kwenye mitandao ya kijamii wameonekana kutofautiana kimawazo na Vdj Jones ambapo wametaka aache ishu ya kutumia jina la Exray kutafutia kiki. Utakumbuka mapema Exray alifunguka kuwa wimbo wake wa “Sipangwingwi” umempa mafanikio makubwa kwani wimbo umempelekea kumiliki gari.

Read More