EXRAY AZIMA TETESI ZA WIMBO WAKE “SIPANGWINGWI” KUPIGWA MARUFUKU

EXRAY AZIMA TETESI ZA WIMBO WAKE “SIPANGWINGWI” KUPIGWA MARUFUKU

Staa wa muziki nchini Exray amekanusha tetesi zinazosambaa mtandaoni kwamba wimbo wake uitwao Sipapangwi umepigwa marufuku kuchezwa kwenye maeneo ya umma. Katika mahojiano yake hivi karibuni Exray amesema madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa ni propaganda zinazosambazwa  na watu wanaotakia mabaya mtandaoni. Msanii huyo wa kundi la Boondocks gang amewataka mashabiki zake wanaendelea kustream wimbo huo kwenye digital platforms mbali mbali mtandaoni kwani wimbo huo hauna matamshi ya chuki kama inavyodhaniwa. Utakumbuka wiki kadhaa iliyopita tume ya uwiano na utangamano nchini ilitoa orodha ya maneno yaliyopigwa marufuku kwenye majukwaa ya kisiasa na neno sipangwingwi ilikuwa moja kati ya maneno hayo.

Read More
 BREEDER LW MBIONI KUACHIA COLLABO YAKE NA EXRAY TANIUA

BREEDER LW MBIONI KUACHIA COLLABO YAKE NA EXRAY TANIUA

Habari nzuri kwa mashabiki wa muziki nchini ni kwamba tutarajie muda wowote ujio wa Collabo kati ya Exray na Rapper Breeder LW. Breeder LW amethibitisha taarifa hiyo kwa mashabiki kupitia mahojiano yake ya hivi karibuni ambapo amewataka mashabiki kukaa mkao wa kula kupokea wimbo huo. Iwapo Breeder Lw na Exray wataachia collabo yao hiyo itakuwa ni kazi yao ya kwanza kufanya pamoja ikizingatiwa kuwa kipindi cha nyuma wamekuwa wakikutana kwenye kazi za wasanii wengine. Ikumbukwe Breeder Lw anafanya vizuri na singo yake mpya “Gin ama Whisky ambayo amemshirikisha Mejja na mpaka sasa video yake ina views million 1.2 kwenye mtandao wa youtube ndani kipindi cha wiki tatu.

Read More
 EXRAY TANIUA APOKEZWA TUZO NA MTANDAO WA YOUTUBE

EXRAY TANIUA APOKEZWA TUZO NA MTANDAO WA YOUTUBE

Msanii wa kundi la Boondocks Gang, Exray Taniua ametunukiwa tuzo ya Silver Play Button na mtandao wa Youtube baada ya kufikisha jumla ya subscribers laki moja kwenye channel yake. Exray ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa Instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia kazi zake za muziki huku akiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi. Channel ya youtube ya Exray ilifunguliwa rasmi Aprili 4 mwaka wa 2017 na mpaka sasa imefikisha zaidi ya watazamaji millioni 11.3 huku ikiwa na jumla ya subscribers 154, 000. Utakumbuka tuzo ya Silver Play button huwa inatolewa kwa wanamuziki au watu maarufu kwenye mtandao wa youtube ambao hujizolea zaidi ya subcribers laki moja.

Read More
 MSANII WA BONDOCKS GANG EXRAY TANIUA ATHIBITISHA UJIO WA KOLABO ZAKE MBILI NA WASANII WA NIGERIA

MSANII WA BONDOCKS GANG EXRAY TANIUA ATHIBITISHA UJIO WA KOLABO ZAKE MBILI NA WASANII WA NIGERIA

Msanii nyota nchini Exray Taniua anazidi kuchana mbuga kimataifa hii ni baada ya kutangaza ujio wa kolabo zake na wasanii nyota nchini Nigeria. Kupitia instastory yake kwenye mtandao wa Instagram Exray amethibitisha kuwa ana kolabo mbili na simi pamoja Mr. Eazi ambapo amewataka  mashabiki zake wampe ushauri ni kolabo gani kati ya wasanii hao aachie kwanza. Hata hivyo baadhi ya mashabiki wamependekeza aachie kolabo zote mbili huku wengine wakimshauri aachia kola yake na Simi kwani moja kati ya wadada ambao muziki wao unawakosha. Huu ni muundelezo mzuri kwa Exray ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akiachia nyimbo bila kupoa.

Read More
 EXRAY TANIUA AWEKA REKODI BOOMPLAY KUPITIA SINGO IITWAYO SIPANGWINGWI

EXRAY TANIUA AWEKA REKODI BOOMPLAY KUPITIA SINGO IITWAYO SIPANGWINGWI

Oktoba 30 mwaka wa 2021 Staa wa muziki nchini Exray Taniua alitubariki na singo inayokwenda kwa jina la Sipangwingwi akiwa amewashirikisha wasanii Sylvia Ssaru na Trio Mio. Goods news ni kwamba Wimbo huo umefanikiwa kufikisha jumla ya streams millioni moja kwenye mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa Boomplay Kenya. Sanjari na hilo wimbo wa  Sipangwingwi pia unazidi kufanya vizuri kwenye mtandao wa youtube kwani mpaka sasa video yake imeweza kutazamwa zaida ya mara millioni 1.9  tangu ipakiwe kwenye mtandao huo. Huu ni muendelezo mzuri kwa  Exray ambaye katika siku za hivi karibuni amekuwa akiachia nyimbo mfululizo bila kupoa.

Read More