MCSK Yaonya Kumbi za Burudani Zinazopuuza Wasanii Walio na Leseni

MCSK Yaonya Kumbi za Burudani Zinazopuuza Wasanii Walio na Leseni

Afisa Mtendaji Mkuu wa Chama cha Hakimiliki ya Muziki Kenya (MCSK), Dkt. Ezekiel Mutua, ametoa onyo kali kwa wamiliki wa kumbi za burudani, hoteli na maeneo ya umma yanayopiga muziki, akiwataka kutoepuka au kuwatenga wasanii walio na leseni halali. Kupitia taarifa aliyotoa kwa vyombo vya habari, Dkt. Mutua alisema kuwa baadhi ya maeneo ya burudani yamekuwa yakikiuka haki za wasanii kwa kupiga nyimbo zao bila kufuata taratibu za leseni, au kwa kuandaa matukio bila kushirikisha wanamuziki waliojisajili kisheria. “Maeneo yanayoendelea kuwasiliti wasanii na kutumia kazi zao bila leseni yako katika hatari ya kupokonywa kibali cha kupiga muziki wenye hakimiliki,” alionya Mutua. Amesisitiza kuwa MCSK itaongeza ukaguzi na kuchukua hatua za kisheria dhidi ya wale wote wanaokiuka sheria za hakimiliki, ili kuhakikisha kuwa wasanii wanalindwa na kunufaika na kazi zao. Onyo hili linajiri wakati ambapo mjadala kuhusu malipo duni kwa wasanii unazidi kushika kasi, huku wasanii wengi wakilalamika kwamba kazi zao zinatumika kibiashara bila wao kufaidika ipasavyo. Chama cha Hakimiliki ya Muziki Kenya kimehimiza waandaaji wa matukio, DJ’s, na wamiliki wa biashara kuhakikisha kuwa wanashirikiana na wasanii walio na leseni na kulipia matumizi ya muziki ili kuunga mkono ukuaji wa tasnia ya muziki nchini.

Read More
 EZEKIEL MUTU AMKINGIA KIFUA ODINGA KWA KUTUMIA WIMBO WA SAUTI SOL KWENYE SHUGHULI ZAKE ZA KISIASA

EZEKIEL MUTU AMKINGIA KIFUA ODINGA KWA KUTUMIA WIMBO WA SAUTI SOL KWENYE SHUGHULI ZAKE ZA KISIASA

Mwenyekiti wa chama cha hakimiliki ya muziki nchini Ezekiel Mutua amefunguka kuhusu utata unaozingira wimbo wa Extravaganza wa kundi la Sauti Sol, uliotumiwa na mrengo wa azimio la umoja kwenye hafla ya kumtambulisha mgombea mwenza wa Raila Odinga. Kupitia mitandao yake ya kijamii Mutua amesema azimio la umoja walifuata taritibu zote za kupata leseni ya kutumia wimbo wa extravangaza kwenye kampeini zao. Mutua ameenda mbali na kudai kuwa amesikitisha namna ambavyo Bodi ya hakimiliki nchini imezua tafrani/hofu miongoni mwa watumiaji wa mitandao ya kijamii kwa kutoa taarifa kinzani juu kutumika kwa wimbo wa extravagaza ikizingatiwa kuwa jambo hilo lilipaswa kutatuliwa kwa njia ya mazungumzo. Hata hivyo amesema katiba ya Kenya imeipa jukumu chama cha hakimiliki ya muziki nchini kukusanya pesa kwa niaba ya wasanii,  hivyo hakuna namna ambavyo watakwenda kinyume na sheria za hakimiliki. Hata hivyo msanii wa Sauti Sol, Bien amesema hawatalegeza msimamo wao wa kuichukulia hatua  kali za kisheria timu ya raila odinga kwa kukiuka hakimiliki ya bendi hiyo licha ya watu kuwabeza kwenye mitandao ya kijamii. Utakumbuka Mei 17 mwaka huu Raila Odinga alidai kuwa walitumia wimbo huo kama njia ya kuionesha upendo kundi la Sauti Sol ambalo limeipeperusha bendera ya Kenya kimataifa      

Read More