META Yapiga Marufuku Wizi wa Maudhui Mitandaoni

META Yapiga Marufuku Wizi wa Maudhui Mitandaoni

Kampuni ya Meta, inayomiliki mitandao ya kijamii ya Facebook, Instagram, na Threads, imetangaza kuwa inaanza kuchukua hatua kali dhidi ya akaunti ambazo zinashiriki au kuchapisha upya (repost) maudhui ya akaunti nyingine bila ruhusa au kibali. Kupitia taarifa rasmi, Meta imesema kuwa sera hii inalenga kulinda haki miliki za watumiaji, kuhamasisha ubunifu wa asili, na kupunguza wizi wa maudhui mtandaoni. Akaunti zitakazobainika kukiuka sera hii zitawekewa vikwazo vya kufikia watumiaji wengine (reach restriction), kusimamishwa kwa muda, au hata kufungiwa kabisa. “Hii ni hatua ya kuhakikisha kuwa watu wanaotumia muda na juhudi zao kuunda maudhui wanapewa heshima na ulinzi wanaostahili,” ilisomeka sehemu ya taarifa hiyo. Watumiaji sasa wanahimizwa kuhakikisha wanapata kibali kabla ya kushiriki tena maudhui ya wengine, hasa ya akaunti za kibiashara, wasanii, au waandishi wa habari. Hatua hii imepokelewa kwa hisia mseto, huku baadhi ya watumiaji wakiiunga mkono kwa kusema inalinda ubunifu, ilhali wengine wakieleza wasiwasi kuwa huenda ikapunguza usambazaji wa taarifa muhimu na burudani mtandaoni. Meta inatarajiwa kuanza kutekeleza hatua hizi kikamilifu katika siku chache zijazo, huku ikiwataka watumiaji kusoma na kuelewa masharti ya matumizi ya mitandao yao kwa kina.

Read More
 Facebook Yatangaza Video Zote Kuwa Reels

Facebook Yatangaza Video Zote Kuwa Reels

Mtandao maarufu wa kijamii, Facebook, umetangaza rasmi kuwa kuanzia sasa video zote zitakuwa katika mfumo wa Reels, hatua inayolenga kuimarisha na kuboresha uzoefu wa watumiaji wake wa video fupi. Kwa mujibu wa taarifa kutoka Facebook, mabadiliko haya yatafanyika kwa lengo la kuendana na mwelekeo wa sasa wa matumizi ya video za muda mfupi zinazopendwa zaidi na watumiaji duniani kote. Reels, ambazo awali zilianzishwa kwenye Instagram, zimekuwa maarufu sana kwa uwezo wake wa kutoa burudani ya haraka na kuendana na mwenendo wa mitandao ya kijamii. Mwenyekiti wa Facebook alisema kuwa mpango huu utawezesha waundaji wa maudhui na watumiaji kupokea na kushiriki video kwa urahisi zaidi, huku pia ukitoa fursa za kukuza ubunifu na kufikia hadhira kubwa zaidi. Mabadiliko haya yatasaidia pia kuboresha uzoefu wa mtumiaji kwa kutoa interface rahisi na zenye mvuto zaidi, ikizingatia hitaji la kuendana na mwenendo wa sasa wa matumizi ya simu za mkononi. Watumiaji wanahimizwa kujiandaa kwa mabadiliko haya ambayo yanatarajiwa kuanza kutekelezwa hatua kwa hatua katika siku za usoni.

Read More
 “CRYPTO” WALLET MPYA YA FACEBOOK YAANZA KUFANYA KAZI

“CRYPTO” WALLET MPYA YA FACEBOOK YAANZA KUFANYA KAZI

Baada ya Facebook kusumbuliwa na fedha ya kidigitali ya Libra, iliamua kuipa jina la “Diem” na kuwekeza katika kutengeneza Wallet ya Novi ambayo itatumika kutuma na kupokea fedha na itaunganishwa na crypto, metaverse, mfumo wa matangazo, na apps za Instagram, Facebook na WhatsApp ambapo watumiaji wataweza kutuma na kupokea fedha bure kwa urahisi. Kwa sasa Wallet (pochi ya kidigitali) ina crypto (stable coin) ya Paxos Dollar ambayo ina thamani sawa na Dola. Mkuu wa Idara ya Facebook inayosimamia Novi Wallet, David Marcus amesema kuna zaidi ya watu Bilioni 1.7 ambao hawana akaunti za kibenki na zaidi ya watu Bilioni 1 hawafurahishwi na mfumo wa mabenki hasa katika makato ya kutuma na kupokea fedha. Facebook imeanza kutoa wallet yake ya Novi kuanza kutumika kwa wakazi wa Marekani na Guatemala. Novi Wallet ni wallet ya Facebook ambayo itakuwa haina makato katika kutuma na kupokea fedha. Ni salama,haikusanyi data na Facebook imejaribu kuweka umakini ili kuepusha sifa mbaya katika kusimamia mfumo huo wa kifedha. Wallet hiyo inatumia coin ya Pax Dollar (USDP) na wiki hii imeshirikiana na Coinbase kuwezesha watumiaji kununua na kuuza Pax Coin kwa kutumia wallet hizo mbili. Wallet ya Novi itakuwa haina makato katika kutuma fedha, ni salama  na inatumia mifumo mikubwa ya kuthibiti usalama na urahisi kwa watumiaji. Facebook inajaribu kuifanya iwe “Wallet ya mitandao ya kijamii”.

Read More
 KAMPUNI YA FACEBOOK KUBADILI JINA LA BRAND YAKE

KAMPUNI YA FACEBOOK KUBADILI JINA LA BRAND YAKE

Baada ya miaka 17 ya kuwepo kwa brand kubwa ya mitandao ya kijamii; Facebook inapanga kubadilisha brand na jina lake mwisho wa mwezi huu. Tetesi zilizovuja mtandaoni zinasema kwamba Mark Zuckerberg atatambulisha jina jipya la kampuni ya Facebook Oktoba 28 katika mkutano wa Annual Connect Conference 2021. Malengo mapya ya Facebook ni kuingia katika teknolojia ya Metaverse na kuacha kuwa tu mtandao wa kijamii. Facebook ina malengo ya kukuza huduma za Instagram, WhatsApp na Uculus; kuhamia katika ulimwengu wa Virtual Reality na Augmented Reality. Facebook haitakuwa kampuni pekee ya teknolojia ambayo imebadili brand yake. Mwaka 2015, Google ilibadilisha muunganiko wa kampuni zake na kuziweka chini ya Alphabet Inc na kuacha kuwa Search Engine tu. Facebook itafanya branding mpya ya kampuni yake na kuweka malengo katika teknolojia ya metaverse ambapo watumiaji wake watawasiliana katika mitandao ya kijamii na katika virtual reality. Kampuni hiyo pia inalenga kuingia katika soko la saa, simu, VR, Metaverse na Games. Hakuna anayefahamu jina la brand mpya ya Facebook, hata wakuu na viongozi wengi wa Facebook hawajaambiwa jina la kampuni kuu ambayo itasimamia social media platform na metaverse.

Read More