FaceTime Kuanzisha Teknolojia ya Kuzuia Video Call Endapo Mtumiaji Atavua Nguo

FaceTime Kuanzisha Teknolojia ya Kuzuia Video Call Endapo Mtumiaji Atavua Nguo

Kampuni ya Apple imeanzisha teknolojia mpya ya usalama katika huduma ya FaceTime, itakayoweza kusitisha simu za video pale ambapo itabainika kuwa mtumiaji amevua nguo au kutumia lugha ya matusi wakati wa mawasiliano. Hatua hii inalenga kulinda watumiaji dhidi ya unyanyasaji wa kingono na maudhui yasiyofaa. Teknolojia hiyo mpya, inayotegemea akili bandia (AI), itaweza kutambua si tu picha za utupu bali pia sauti zenye matusi au lugha ya kudhalilisha. Endapo mfumo huo utagundua maudhui hayo, FaceTime itakatiza mazungumzo mara moja na kutoa arifa kwa mtumiaji aliyeathirika, huku ikimpa chaguo la kuripoti tukio hilo. Apple imesema kuwa uchakataji wa data utafanyika moja kwa moja kwenye kifaa (on-device processing), ili kulinda faragha ya mtumiaji bila kutuma data hizo kwenye seva za kampuni. Watumiaji wengi wamesifia hatua hiyo wakisema inasaidia kudhibiti unyanyasaji wa kimtandao, hasa kwa watoto na watu wazima wanaolengwa na wanyanyasaji kupitia simu za video. Maboresho haya mapya yanatarajiwa kuzinduliwa rasmi kupitia toleo la hivi punde la iOS, litakalotoka msimu wa vuli (Fall) mwaka huu. Apple inatarajia FaceTime kuendelea kuwa mojawapo ya majukwaa salama zaidi ya mawasiliano ya video duniani.

Read More