RAPPER FETTY WAP ATUPWA JELA KWA KOSA LA KUMILIKI DAWA ZA KULEVYA
Rapa kutoka Marekani Fetty Wap yupo Gerezani akisubiri tarehe ya hukumu yake kwenye Kesi ya kumiliki na kusambaza dawa za kulevya aina ya Cocaine. Kosa hilo linabeba hukumu ya chini ya miaka 5. Agosti 22 mwaka huu, Fetty Wap alikiri mbele ya Mahakama kuwa na hatia ya kutekeleza kosa la kumiliki na kusambaza Gram 500 za dawa za kulevya aina ya Cocaine. Oktoba 2019, Fetty Wap pamoja na wenzake sita walikamatwa na dawa hizo nje ya Tamasha la Rolling Loud.
Read More