FIFA yatangaza rekodi ya usajili

FIFA yatangaza rekodi ya usajili

Shirikisho la soka Duniani FIFA limetangaza kuwa dirisha dogo la usajili la mwezi januari 2025 limeweka rekodi ya matumizi makubwa ya pesa kwa ongezeko la asalimia 58 ukilinganisha na dirisha dogo la usajili lililopita la mwaka 2024. FIFA imeweka wazi kuwa katika shughuli zote za usajili zilizofanywa na vilabu Duniani kote kwenye dirisha Dogo lla mwaka huu 2025 kiwango cha pesa kilichotumika ni pesa za marekani Dola Bilioni 2.35 ambayo ni zaidi ya Trilioni 6 kwa pesa ya Tanzania. Takwimu za FIFA zimeonyesha jumla ya sajili 5,863 zimefanyika kwa njia rasmi za FIFA kwenye dirisha dogo kati ya Januari 1, 2025 hadi Februari 4, 2025. Ikiwa ni ongezeko la asilimia 19.1 ya rekodi ya awali ya idadai kubwa ya wachezaji waliosajiliwa kwenye dirisha dogo.

Read More
 FIFA yakataa ombi la Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

FIFA yakataa ombi la Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky

Kuelekea fainali ya mchezo wa Kombe la Dunia Jumapili hii unaozikutanisha timu ya Taifa ya Argentina na Ufaransa, Shirikisho la Soka Ulimwenguni (FIFA) limekataa ombi la Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky kutaka kabla ya mchezo huo kuanza, ichezwe video yake uwanjani hapo ili kuhamasisha amani. Imeelezwa kwamba Rais wa Ukraine Volodymyr Zelensky aliomba jambo hilo FIFA huku akitaka kuonekana katika video hiyo akitoa ujumbe wa kuhamasisha amani wakati huu Ukraine ikiwa katika vita kati yake na Urusi. Taarifa za ndani kutoka vyanzo mbalimbali vya kuaminika zinaeleza kuwa, FIFA wamemkatalia Rais huyo wa Ukraine ombi hilo pasipo kumpa sababu za kukataa.

Read More