Fik Fameica: Pallaso Ni Shabiki Tu, Si Mlezi Wangu Kimuziki

Fik Fameica: Pallaso Ni Shabiki Tu, Si Mlezi Wangu Kimuziki

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Fik Fameica amevunja ukimya na kukanusha vikali madai ya msanii mwenzake Pallaso, ambaye kwa muda mrefu amekuwa akidai kuwa alihusika pakubwa katika kukuza safari yake ya muziki. Hii ni baada ya Pallaso kudai kuwa alimtoa Fik Fameica kwenye mitaa ya Kawempe, na kumtambulisha kwenye muziki, na hata kumsaidia kifedha alipokuwa anaanza safari yake ya muziki. Hata hivyo, Fik Fameica kwenye mahojiano yake hivi karibuni ameyakana madai hayo akisema kwamba Pallaso hajawahi kutoa mchango wowote wa maana katika mafanikio yake. Alieleza kuwa Pallaso alikuwa tu shabiki kama walivyo mashabiki wake wengine. “Pallaso aliwadanganya. Hajawahi changia chochote katika safari yangu ya muziki. Alikuwa tu shabiki wangu, si zaidi ya hapo,” alisema Fameica katika mahojiano na runinga moja nchini Uganda. Fameica alisisitiza kuwa yeye ni msanii aliyejijenga mwenyewe (self-made), na kwamba mafanikio yake yalianza mara ya kwanza tu alipoingia studio. “Mimi ni msanii aliyejijenga. Mara ya kwanza niliingia studio, nilitoa kibao ‘Pistol’ ambacho kilipokelewa vizuri,” aliongeza. Fik Fameica alipata umaarufu mkubwa mwaka 2018 kupitia wimbo wake maarufu “Kutama”, na tangu wakati huo amekuwa akitoa nyimbo kali mfululizo na kumuweka katika nafasi ya juu kama mmoja wa wasanii bora zaidi katika tasnia ya muziki Afrika Mashariki.

Read More
 Album ya Fik Fameica, “King Kong” yakamata namba moja Apple Music

Album ya Fik Fameica, “King Kong” yakamata namba moja Apple Music

Rapa kutoka nchini Uganda Fik Fameica ameendelea kutikisa katika vichwa vya habari kwenye mitandao mbalimbali ya kijamii kwa album yake ya King Kong. Kwa mujibu wa takwimu album ya rapa huyo King Kong imevunja rekodi na kuwa ya kwanza katika mtandao wa kusikiliza muziki  wa “Apple” kwa upande wa afrika ikiipiku album ya Burna Boy, Love Denim. Fik Fameica ametumia ukurasa wake wa mtandao wa kijamii wa instagram kuwashukuru mashabiki zake kwa upendo ambao wanazidi kumuonyesha kupitia album yake mpya huku akiahidi kuendelea kuwapa burudani zaidi. Album ya King Kong iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki wa Fik Fameica imeingia sokoni rasmi  Oktoba 29, mwaka wa 2022 ikiwa na jumla ya mikwaju 18.

Read More
 Fik Fameica aachia rasmi Tracklist ya Album yake mpya

Fik Fameica aachia rasmi Tracklist ya Album yake mpya

Nyota wa muziki wa Dancehall Kutoka nchini Uganda Fik Fameica ameachia rasmi orodha ya ngoma zinazopatikana kwenye Album yake mpya inayokwenda kwa jina la “King Kong” Fik Fameika amethibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram kwa kuonesha tracklist hiyo yenye jumla ya mikwaju 14 ya moto. Album hiyo imewakutanisha mastaa kama Eddy Kenzo, Geosteady, Bruce Melody, Vanessa Mdee na Mozelo Kids. King Kong ambayo ni album ya kwanza kwa mtu mzima Fik Fameica inatarajiwa kuingia sokoni rasmi Ijumaa hii Oktoba 7 mwaka 2022.

Read More
 PROMOTA WA LONDON ATISHIA KUICHUKULIA HATUA KALI LEBO YA SWANGZ AVENUE

PROMOTA WA LONDON ATISHIA KUICHUKULIA HATUA KALI LEBO YA SWANGZ AVENUE

Promota wa Uganda wanayoishi mjini London Maama Africa ametishia kuhakikisha kuwa waimbaji wote wa Swangz Avenue wamepigwa marufuku kusafiri hadi London, lebo hiyo isipomlipa fidia ya euro 65000. Promota hao anadai kuwa alilipa Euro 5000 ili Winnie Nwagi atumbuize London lakini siku ya tukio, Nwagi pamoja na Fik Fameika walikataa kutoa burudani kwa mashabiki hadi usiku wa manane wakati walipotumbuiza nyimbo chache. Lakini pia wasanii hao walivunja mkataba na kutumbuiza kwenye shoo nyingine iliyopewa jina la “Chill and Grill” kwa kutumia kibali chake cha kazi, kitu ambacho anaona si cha kingwana. “Nataka kuwafundisha uweledi waimbaji wa Uganda. Nililipa na kugharamia kila kitu kwa Winnie Nwagi, lakini alienda mbali zaidi na kutumbuiza katika hafla nyingine bila idhini yangu,” alisema katika mahojiano na MwanaYouTube. Promota hao wameongeza, “Aliimba nyimbo chache tu baada ya kuchelewa kufika. Nimeiandikia Swangz avenue kuhusu kitendo hicho na ninatarajia jibu kabla ya Jumatatu la sivyo nitahakikisha kuwa wasanii wake wanapigwa marufuku kutumbuiza London.” Hata hivyo Maama Africa wanahusisha kuporomoka kwa onyesho hilo na vitendo visivyo vya kitaaluma vya Winnie Nwagi.

Read More
 FIK FAMEICA AWATOLEA UVIVU WASANII WA UGANDA, ACHANENI WIVU PIGENI KAZI

FIK FAMEICA AWATOLEA UVIVU WASANII WA UGANDA, ACHANENI WIVU PIGENI KAZI

Msanii  wa muziki kutoka uganda Fik Fameica amewatolea uvivu wasanii wa uganda wanaopiga vita wasanii wa nigeria kwenye tasnia ya muziki nchini humo. Katika mahojiano yake hivi karibuni Hitmaker huyo wa Kanzunzu amewataka wasanii wa uganda kuacha kasumba ya kuwachukia wasanii wa nigeria na badala yake wajifunze kutoka kwao namna ya kufanikiwa kimuziki kwani ni wasanii ambao wanafanya vizuri duniani. Fameica ambaye alipata shavu ya kufanya kazi na kampuni ya empewa africa inayomilikiwa na Mr. Eazi ametoa changamoto kwa wasanii wa uganda kuwekeza kwenye muziki wao badala ya kutoa muziki usiokidhi viwango vya kimataifa “Nigerian music is popular worldwide. Those guys have done well. Instead of fighting them, we should embrace and learn from them,” amesema Fameika. Utakumbuka Wasanii wengi nchini Uganda wamekuwa wakiwalaumu mapromota wa muziki kwa kuwazingatia sana wasanii wa nigeria kwenye shoo zao huku wakiwatenga wasanii wa ndani jambo ambalo walihoji kuwa ni njia ya kuua muziki wao.

Read More
 FIK FAMEICA ADOKEZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI

FIK FAMEICA ADOKEZA UJIO WA TAMASHA LAKE LA MUZIKI

Mwanamuziki kutoka Uganda Fik Fameica ameweka wazi tarehe ambayo tamasha lake la muziki litakalofanyika mwezi Agosti mwaka huu. Kupitia ukurasa wake wa twitter Fameica amesema tamasha lake liitwalo ” Fik Fameica live in concert” litafanyika Agosti 26 mwaka huu katika hoteli ya Africana jijini Kampala. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Kanzunzu”  licha ya kutoweka wazi kiingilio na wasanii watakaomsindikiza kwenye tamasha lake la muziki, amesema ataendelea kutoa taarifa zaidi kwa mashabiki zake kwenye mitandao yake ya kijamii. Hii sio mara ya kwanza kwa Fik Fameica kuandaa tamasha lake mwenyewe mwaka wa 2018 alifanya tamasha liitwalo “My Journey” huko Cricket Oval Lugogo nchini Uganda ingawa haikupata mapokezi mazuri

Read More
 FIK FAMEICA ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WA AFRIKA MASHARIKI KUJA NA SOUND YA MUZIKI WAO

FIK FAMEICA ATOA CHANGAMOTO KWA WASANII WA AFRIKA MASHARIKI KUJA NA SOUND YA MUZIKI WAO

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Fik Fameica ametoa wito kwa wasaniii kutoka Uganda, Kenya na Tanzania kuungana kwa ajili ya kuja na sound itakayotambulisha muziki wa Afrika Mashariki kimataifa. Katika mahojiano yake hivi karibuni Fik Fameica amesema muziki wa Nigeria uitwao Afro-Beat umeufunika muziki wa Afrika mashariki kuweza kutambulika duniani kutokana ukanda huu kukosa jina linalowakilisha muziki wake. Hata hivyo Hitmaker huyo wa ngoma ya “Property” ametoa changamoto kwa wasanii wa Afrika Mashariki kuja na jina litakalotenganisha muziki wao na wa mataifa mengine ya Afrika kama ilivyo kwa muziki wa Amapiano kutoka Afrika kusini. Fik Fameica anaungana na mtu mzima Harmonize ambaye amekuwa moja kati ya wasanii ambao wamekuwa wakishinikiza muziki wa Afrika Mashariki uwe na jina moja kama ilivyo kwa muziki wa nigeria na Afrika kusini.

Read More