FC Talanta Yaizima Tusker FC, Mbio za Ubingwa zapata Pigo

FC Talanta Yaizima Tusker FC, Mbio za Ubingwa zapata Pigo

Mechi saba za Ligi Kuu ya Soka Nchini Kenya zilipigwa hapo jana na kuleta mabadiliko muhimu kwenye msimamo wa ligi. Ulinzi Stars walilazimishwa sare ya bao moja kwa moja dhidi ya Posta Rangers katika uwanja wa Ulinzi Complex. Tusker FC wakajikuta pabaya walipopoteza mabao mawili kwa bila mikononi mwa FC Talanta, matokeo yanayowapunguzia kasi kwenye mbio za ubingwa. Kakamega Homeboyz waliibuka na ushindi wa mabao 2 kwa 1 dhidi ya Kenya Police FC katika uwanja wa Bukhungu, huku Shabana FC wakiwafunga Bidco United kwa mabao kama hayo kwenye uwanja wa Gusii. Mara Sugar na Bandari FC walitoshana nguvu kwa sare tasa, huku Murang’a SEAL wakipata ushindi wa mabao 2 kwa 0 dhidi ya Sofapaka. Na katika uwanja wa Nyayo, AFC Leopards waliwashusha Mathare United kwa mabao 3 kwa 1. Leo, Alhamisi, Kariobangi Sharks watakuwa nyumbani dhidi ya KCB katika uwanja wa Kasarani, huku Gor Mahia wakipambana na Nairobi City Stars kwenye uwanja wa Nyayo. Mechi hizi mbili zinatarajiwa kuathiri mwelekeo wa msimamo wa ligi kadri msimu unavyoelekea ukingoni

Read More
 Matumaini ya Police FC kusalia kileleni mwa Ligi Kuu ya soka FKF yapata pigo

Matumaini ya Police FC kusalia kileleni mwa Ligi Kuu ya soka FKF yapata pigo

Matumaini ya Police FC kusalia kileleni mwa ligi kuu ya soka nchini FKF yalipata pigo baada ya kutoka sare na Sofa Paka bao moja kwa moja katika mechi iliyochezwa uwanjani Kenyatta, mjini Machakos. Donata Okello aliipa Sofa Paka bao la uongozi dakika 37 na kulazimisha matokeo hayo kufikia wakati wa mapumziko. Hata hivyo katika kipindi cha pili Brian Okoth aliisawazishia polisi katika dakika ya 87 huku mechi hiyo ikamalizika kwa sare ya goli moja kwa moja. Kwenye mechi zingine zilizochezwa leo Bandari FC ilipata ushindi wa mabao matatu kwa mawili dhidi ya Muranga Seal, Shabana FC na Kariobangi Sharks zikatoka sare tasa, FC Leorpards iliilaza Nairobi City Stars bao moja kwa nunge nayo Tusker FC ikatoka sare kapa na KCB.

Read More