Flaqo Awatahadharisha Vijana: “Acheni Kuabudu Mapenzi ya Mitandaoni”

Flaqo Awatahadharisha Vijana: “Acheni Kuabudu Mapenzi ya Mitandaoni”

Mchekeshaji maarufu nchini Kenya, Flaqo Raz, ameibua mjadala mitandaoni baada ya kutoa ujumbe mzito kwa mashabiki na hasa vijana kuhusu mapenzi yanayoonyeshwa mitandaoni. Kupitia ukurasa wake wa Instagram, Flaqo alitoa tahadhari dhidi ya kupumbazwa na picha na video za wapenzi maarufu ambazo zinaonekana kuwa za kufurahisha na za kuvutia. Katika ujumbe wake, Flaqo alisema wazi kwamba watu wanapaswa kutambua kuwa maisha ya mapenzi yanayoonekana mitandaoni si halisi kama wengi wanavyodhani. “Stop admiring love/couples you see online. It’s a lie. Everything you see online is rehearsed,” aliandika Flaqo. Mchekeshaji huyo ambaye anafahamika kwa ubunifu wa kuigiza wahusika wengi katika video zake, alisisitiza kwamba sehemu kubwa ya maisha yanayoonyeshwa mtandaoni yamepangwa kwa ajili ya kuwavutia watu na si lazima yawe ya kweli. Alisema kuwa wengi huishia kujihisi duni au kutokuwa na thamani kwa sababu wanalinganisha maisha yao na taswira zisizo halisi. “Mitandaoni ni kama jukwaa la maigizo. Wengi hupost wanachotaka watu waone, siyo hali halisi. Mapenzi ya kweli hayana haja ya kamera,” aliongeza katika mahojiano ya awali. Flaqo anatoa wito wa kujenga maisha halisi yenye msingi wa mawasiliano, uaminifu na heshima badala ya kufuata tu kile kinachovuma mtandaoni. Katika dunia ya “likes” na “follows”, anawakumbusha mashabiki kwamba furaha ya kweli haipo kwenye kamera, bali kwenye maisha halisi yanayojengwa kwa bidii na kuelewana. “Mpende mtu kwa sababu ya uhalisia wake, si kwa sababu ya jinsi wanavyoonekana mtandaoni,” anasema Flaqo ujumbe ambao wengi wanaona kuwa ni muhimu zaidi sasa kuliko wakati wowote ule. Ujumbe huu umepokelewa kwa hisia tofauti na mashabiki. Wengi walimuunga mkono, wakisema kwamba vijana wengi wanateseka kisaikolojia kwa sababu ya matarajio ya mapenzi yaliyojengwa kutokana na kile wanachokiona kwenye Instagram, TikTok na YouTube.

Read More
 Flaqo Azima Uvumi wa Mapenzi na Trish Khalid

Flaqo Azima Uvumi wa Mapenzi na Trish Khalid

Mchekeshaji maarufu nchini Kenya, Flaqo Raz, amekanusha madai ya kuwahi kuwa katika uhusiano wa kimapenzi na mwigizaji na mrembo maarufu Trisha Khalid. Kupitia mahojiano aliyofanya hivi majuzi, Flaqo alieleza kwa uwazi kuwa madai hayo hayana ukweli wowote. “It’s a lie, it never happened,” alisema Flaqo kwa msisitizo, akijibu uvumi uliokuwa ukienea mitandaoni kuhusu uwepo wa uhusiano wa kimapenzi kati yake na Trisha. Kwa muda mrefu, mashabiki na watumiaji wa mitandao ya kijamii wamekuwa wakihusisha wawili hao, wakitumia picha na video walizowahi kufanya kazi pamoja kama ushahidi wa mapenzi kati yao. Hata hivyo, Flaqo amesema walikuwa tu marafiki wa kawaida waliokuwa wakishirikiana kwenye kazi na miradi ya kisanaa. “Watu wana tabia ya kuchukulia kila interaction mtandaoni kama ishara ya uhusiano wa kimapenzi, lakini si kweli. Sijawahi toka na Trisha,” aliongeza. Trisha Khalid bado hajajibu rasmi kuhusu kauli ya Flaqo, ingawa awali aliwahi pia kukanusha uvumi huo kupitia Insta Stories zake. Mashabiki wamepokea taarifa hii kwa hisia mseto, huku wengine wakisema walikuwa na matumaini kwamba wawili hao walikuwa wapenzi, kutokana na muonekano wa ukaribu wao. Flaqo, ambaye pia ni muigizaji, mtayarishaji na msanii wa muziki, aliwataka mashabiki wake kuzingatia kazi na ubunifu wake badala ya maisha yake ya kibinafsi.

Read More