Rapa Flo Rida ashinda kesi dhidi ya kampuni ya Celsius
Mwanamuziki kutoka Marekani Flo Rida ameshinda shtaka lake dhidi ya Kampuni ya vinywaji vya kuongeza nguvu, Celsius. Kampuni hiyo ya Energy Drink itamlipa Flo Rida kiasi cha zaidi ya KSh. billioni 10 kama fidia kwa kuwahi kumvunjia mkataba katikati ya makubaliano. Awali alikuwa akiidai kampuni hiyo kiasi cha Ksh million 3.7 lakini kutokana na Kampuni hiyo kuwa kubwa zaidi na kupata faida kubwa hasa kupitia yeye na nyimbo zake wakati akiitangaza tangu 2014, aliongeza kiasi hadi kufikia billion 10.
Read More