FOBY ALILIA PENZI LA ZUCHU KUTOKA WCB

FOBY ALILIA PENZI LA ZUCHU KUTOKA WCB

Msanii wa Muziki wa Bongo Fleva Foby ameshindwa kabisa kuficha hisia zake kwa Mrembo Zuchu kutoka WCB. Kupitia Ukurasa wake wa Instagram Foby  ameamua kuonesha hisia zake kwa Zuchu kwa kuweka jumbe mbalimbali zikielezea jinsi Anamzimia. Foby amebainisha kuwa kuna kipindi aliishi kwa ugumu baada ya kusambaa kwa taarifa zikidai Zuchu anataka kuolewa. Hata hivyo ameomba kuwepo na Wizara ya Mahusiano akihofia kuumia na kuja kufa kwa kulikosa penzi la mrembo huyo. “Hakuna kipindi nimeishi kwa ugumu kama kile kipindi wanasema anataka kuolewa,Roho yangu ilikuwa kama ya kuazima,Mi niliamua kum_Unfollow kwasababu nikiona picha yake tu mshtuko naoupata utasema nipo nchi ya ukrain, kwani hakuna wizara yoyote inayoweza kupatanisha watu nchini kwetu? Pls kuwe na wizara ya mahusiano na mapenzi haki vile kuna watu tunaumia na tutakuja kufa tumesimama, Nyie huyu mtoto mi atakuja kuniua huyu,”  Ameandika FOBY kupitia Instagram. Hajajulikana kama kweli Foby anahusudu penzi la zuchu au anatumia jina lake kutengeneza mazingira ya kuzungumziwa mtandaoni.

Read More
 FOBY AANDIKA BARUA YA WAZI KWA WADAU WA MUZIKI WA BONGOFLEVA

FOBY AANDIKA BARUA YA WAZI KWA WADAU WA MUZIKI WA BONGOFLEVA

Mwanamuziki na mwandishi wa muziki kutoka Tanzania, msanii Foby ameandika barua ya wazi kwa mashabiki wa Bongofleva, Basata na Tuma (Chama cha Muziki wa Kizazi kipya) kwa ajili ya kuomba ridhaa ya kuachia wimbo wake mpya kabla ya mwezi huu kuisha. Kwenye barua hiyo aliyoposti kupitia ukurasa wake wa instagram, Foby ameeleza kwamba mara zote amekuwa akitoa nyimbo kali zenye kuelimisha jamii na kutumia tafsida ila kwenye wimbo wake huu mpya ameomba kusamehewa kwani na yeye anataka hela. Hitmaker huyo wa ngoma ya “Ode” amebainisha kuwa ana nyumba yake anataka kuimalizia. Foby kwenye maelezo yake ya mwishoni katika barua hiyo ametaka majibu ya alichokieleza na endapo yatachelewa amedai kuachia wimbo huo hata leo.

Read More
 FOBY AUPONDA UWEZO WA MARIOO KWENYE MUZIKI WA BONGOFLEVA

FOBY AUPONDA UWEZO WA MARIOO KWENYE MUZIKI WA BONGOFLEVA

Msanii wa Bongofleva Foby amefunguka kuwa mkali wa ngoma ya “Beer tamu” Marioo hawezi kuvikwa taji la Ufalme wa muziki wa kizazi kipya nchini Tanzania. Kupitia mahojiano aliyoyafanya hivi karibuni, mwanamuziki huyo amedai kwamba Marioo hawezi kuwa mfalme wa muziki wa Bongofleva ikiwa anaimba muziki wa Amapiano, kwani mfalme anatakiwa kukuza na kufanya mziki wao wa nyumbani na sio kuiga muziki kutoka mataifa mengine. HitMaker wa ngoma ya “Ode” amechukizwa na kitendo cha rapa Damian Sol kumkana hadharani kwamba hamfahamu kwa kusema kuwa rapa huyo amewavunjia heshima vyombo vya habari ambavyo vimekuwa vikipiga nyimbo zake ikizingatiwa kuwa wamekutana mara nyingi kwenye matamasha mbali mbali ya muziki. Ikumbukwe Foby kwa sasa anafanya vizuri kwenye Digital Platforms mbali mbali na EP yake iitwayo ME, MYSELF & 1 ambayo aliiachia rasmi mwishoni mwa mwaka wa 2021 ikiwa na jumla ya mikwaju 5 ya moto.

Read More