Kendrick Lamar ashinda Tuzo ya Msanii Bora wa  Hiphop kwenye BET Hip-Hop Awards 2022

Kendrick Lamar ashinda Tuzo ya Msanii Bora wa Hiphop kwenye BET Hip-Hop Awards 2022

Rapa Kendrick Lamar ameibuka mshindi wa kipengele cha Hip-Hop Artist Of The Year kwenye Tuzo za BET Hip-Hop 2022 ambazo zinatolewa usiku wa kuamki leo nchini Marekani. Kendrick Lamar pia ameondoka na ushindi kwenye vipengele vya Lyricist Of The Year, Best Hip Hop Video “Family Ties”, Best Live Performer na Hip Hop Album Of The Year (Mr. Morale & The Big Steppers) Kwa upande mwingine Rapa 50 Cent ameibuka mshindi wa Tuzo ya ‘Hustler Of The Year’ akiwaangusha DJ Khaled, Drake, Cardi B, Jay-Z, Kanye West na Megan Thee Stallion. Kolabo ya Future, Tems na Drake “Wait For You” imeshinda Tuzo ya Best Collaboration kwenye Tuzo za BET Hip Hop 2022.

Read More
 FUTURE AUZA HAKI ZA NYIMBO ZAKE KWA KAMPUNI YA INFLUENCE MEDIA PARTNERS

FUTURE AUZA HAKI ZA NYIMBO ZAKE KWA KAMPUNI YA INFLUENCE MEDIA PARTNERS

Rapa kutoka Marekani Future ameripotiwa kuuza haki za nyimbo zake za kuanzia mwaka 2004 hadi 2020 kwa kampuni ya Influence Media Partners. Tovuti za Variety na Billboard zimeripoti, dili hilo linatajwa kuwa na thamani ya kuanzia millioni 7 hadi 9 za Kenya. Catalog iliyouzwa na Future ina jumla ya nyimbo 612 ikiwemo kolabo za wakali kama Drake, Kendrick Lamar, Rihanna na The Weeknd. Mwaka 2022 kampuni ya Influence Media Partners ilitumia kiasi cha billioni 36 kununua haki za nyimbo za Bruno Mars, Dua Lipa, Ariana Grande na Justin Bieber.

Read More