Gen Z Goliath Afunguka kwa Uchungu Baada ya Kushambuliwa

Gen Z Goliath Afunguka kwa Uchungu Baada ya Kushambuliwa

Kijana aliyejipatia umaaurufu nchini Kenya kupitia kimo chake, Gen Z Goliath, ameibuka na kueleza kwa masikitiko makubwa kuhusu tukio la kushambuliwa kwake pamoja na meneja wake, Francis Juma, wakati wa mechi ya kandanda kati ya FIFA Best FC na Bundes FC katika uwanja wa NCC, Kawangware. Kupitia ujumbe wa hisia alioweka mitandaoni, Goliath ambaye pia content creator alisema nia yake kuu ilikuwa ni kusaidia kukuza vipaji vya soka mashinani na kuunga mkono vijana kupitia mchezo huo, lakini mambo yaligeuka na kuwa vurugu.  “Ilikuwa kwa ajili ya upendo kwa soka la mashinani kusaidia mchezo wetu na kuinua wachezaji wa hapa nyumbani. Kwa bahati mbaya, mambo yaligeuka vurugu wakati wa mechi kati ya FIFA Best na Bundes FC. Wahuni walivamia gari langu aina ya Pearl TX na kumshambulia meneja wangu Francis Juma,” alisema. Kulingana na Goliath, genge hilo la wahuni waliiba KSh 100,000 na vitambulisho vya meneja wake, ingawa kwa bahati nzuri, Juma aliweza kuokoa simu yake. Goliath alisisitiza kuwa soka linapaswa kuwa kiungo cha umoja na si uwanja wa machafuko. “Soka ni kuhusu umoja, si fujo. Mimi hujitokeza kusaidia kadri niwezavyo, lakini lazima tuelewane hata nyakati ngumu. Tukio hili halipaswi kurudiwa,” aliongeza. Pia aliwaomba watu wenye moyo wa huruma kusaidia kurudisha kitambulisho cha meneja wake ikiwa watakikuta, akisema ni muhimu kulinda roho ya mchezo wa soka katika jamii. Tukio hilo limezua masikitiko makubwa mitandaoni, huku wapenzi wa michezo, mashabiki na wanaharakati wa kijamii wakimtaka Goliath kuendelea na juhudi zake japo kwa tahadhari zaidi, huku wakilaani vikali tabia ya vurugu kwenye viwanja vya mashinani. Polisi bado hawajatoa taarifa rasmi kuhusu tukio hilo, lakini mashinikizo kutoka kwa umma huenda yakachochea hatua kuchukuliwa dhidi ya wahusika.

Read More
 Director Trevor Ampongeza Bien kwa Kumlipa Vizuri GenZ Goliath Katika Video Mpya ya Muziki

Director Trevor Ampongeza Bien kwa Kumlipa Vizuri GenZ Goliath Katika Video Mpya ya Muziki

Mkurugenzi Mkuu wa Watayarishaji wa Maudhui ya Kidijitali nchini Kenya, Director Trevor, amemsifu msanii Bien kwa kumuonesha heshima ya hali ya juu Gen Z Goliath kwa kumlipa vizuri na kumhudumia ipasavyo kwa ajili ya kuonekana kwa muda mfupi kwenye video ya muziki. Kupitia mitandao ya kijamii, Director Trevor ameweka wazi kuwa Bien alifuata taratibu zote za kazi kwa kulipa kiwango kamili cha malipo, kugharamia usafiri wa Goliath kwa kutumia gari la kifahari aina ya Toyota LX570, pamoja na malazi ya kiwango cha juu wakati wa kutayarisha video ya wimbo wake mpya “All My Enemies Are Suffering” Hii ni tofauti na matukio ya awali ambapo wasanii na waigizaji chipukizi walilalamika kutolipwa au kupuuzwa baada ya kuchangia mafanikio ya kazi mbalimbali za burudani. Mashabiki wengi wamelipongeza tukio hilo wakisema kuwa ni mfano wa kuigwa kwa wasanii wakubwa kuonyesha heshima na kuthamini mchango wa vipaji vinavyochipuka. Aidha, hatua hiyo imeibua matumaini kwa vijana wengi kuwa na imani na kazi yao huku wakijua kuwa juhudi zao zinaweza kutambuliwa na kuthaminiwa kikamilifu. Video ya wimbo mpya wa Bien,“All My Enemies Are Suffering” umewavutia wengi si tu kwa ubora wa maudhui bali pia kwa jinsi ulivyowajumuisha majina maarufu kama DJ Shiti na Gen Z Goliath, ambao wameongeza ucheshi na mvuto katika video hiyo.

Read More