Msanii Parroty Aingia Kwenye Bifu Kali na Militan Baada ya Kunyoa Dreadlocks Zake Bila Ridhaa
Msanii Parroty ameingia kwenye bifu kali na mwenzake Militan kufuatia tukio la kushangaza lililotokana na mzaha wa soka. Parroty, ambaye ni shabiki mkubwa wa Manchester United, awali alitania kuwa angenyoa dreadlocks zake endapo timu yake ingepoteza dhidi ya Tottenham. Baada ya United kufungwa 1-0, hali ilichukua mkondo mpya. Mzaha huo sasa umegeuka kuwa chanzo cha mgogoro mkubwa baada ya Militan kumvamia Parroty na kumnyoa dreadlocks zake bila idhini. Paroty, kupitia mitandao ya kijamii, alielezea hasira na kukerwa kwake na tukio hilo, akilitaja kama udhalilishaji wa hali ya juu. “Hii imevuka mpaka. Sio kila kitu ni mchezo. Sikutegemea nishambuliwe kwa sababu ya maneno ya mzaha,” alisema Paroty, akionya kuwa iwapo watakutana na Militan ana kwa ana, huenda mambo yakaenda kombo. Mashabiki wameingia kwenye malumbano, baadhi wakidai Parroty alipaswa kutimiza ahadi yake, huku wengine wakimtetea wakisema tukio hilo lilikiuka heshima na haki za mtu binafsi. Kwa sasa, Militan bado hajajibu hadharani, huku mvutano ukizidi kuongezeka na tasnia ya burudani ikisubiri kuona hatma ya bifu hilo linalozidi kushika kasi.
Read More