Geoffrey Mosiria Atoa Wito wa Msamaha Kati ya Director Trevor na Eve Mungai
Mchambuzi wa masuala ya mitandaoni, Geoffrey Mosiria, ametoa rai kwa Director Trevor kumsaamehe na kumsaidia aliyekuwa mpenzi wake, Eve Mungai, akisisitiza kuwa wawili hao wanapaswa kuzingatia maisha ya sasa na mipango ya baadaye, badala ya kuzidi kushikilia yaliyopita Kupitia mitandao yake ya kijamii, Mosiria amesema kuwa lawama na kejeli zinazotokana na habari za uongo mitandaoni haziwezi kusaidia chochote, bali ni busara wawili hao waweke kando tofauti zao na kuendelea mbele. Kwa kutoa wito wake, Mosiria amesema mashabiki wanapaswa kutambua kuwa maisha binafsi ya wasanii na wanaburudishaji ni sehemu ya safari zao, na kwamba ni vyema kuunga mkono badala ya kuongeza shinikizo kupitia habari zisizo sahihi. Mosiria alitoa kauli hiyo baada ya posti mbili feki kusambaa mitandaoni na kuibua mjadala kuhusu uhusiano wa wawili hao. Katika moja ya posti hizo bandia, ilidaiwa kuwa Mungai amemuomba radhi Trevor na kutaka warudiane, huku nyingine ikimnukuu akijutia uamuzi wa kuachana naye na kuwaonya mashabiki dhidi ya ushauri mbaya wa mtandaoni.
Read More