Geosteady akanusha kurudiana na baby mama wake Prima Kardash

Geosteady akanusha kurudiana na baby mama wake Prima Kardash

Msanii kutoka nchini Uganda Geosteady amekanusha kurudiana na baby mama wake Prima Kardash kufuatia uvumi unaosamba mtandaoni kuwa wawili hao wanatoka kimapenzi. Kwenye mahojiano na karibuni yake amesema ukaribu wao ulikuwa ni kwa ajili ya kuitangaza show yake itakayofanyika leo aliyoipa jina “Dine With Geosteady” “Alionekana tu kwa video yangu. Hakuna kitu kingine zaidi ya hiyo. Tuna ukaribu kwa sasababu ananisaidia kutangaza show yangu. Sisi sio wapenzi”, Alisema. Geosteady na Prima Kardashi ambao wana watoto watatu kwa pamoja walivunja mahusiano yao miaka mitatu iliyopita na kila mmoja akaingia kwenye mahusiano mengine. Prima alikuwa kwenye mahusiano na Mr.Henrie lakini wakavunja mahusiano yao huku Geosteady akianzisha mahusiano na mrembo aitwayo Hindu kisha baadae akahamia kwa Minaj ambaye wamezaa mtoto mmoja.

Read More
 Sina mpango wa kumuoa Prima Kardash – Geosteady

Sina mpango wa kumuoa Prima Kardash – Geosteady

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Geosteady ameamua kutoa ya moyoni kuhusu hatma ya uhusiano wake na mzazi mwenzie Prima Kardash. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni amesema hana mpango wa kufunga ndoa hivi karibuni na Baby Mama wake huyo. Kulingana na Hitmaker huyo wa “Sembera”, alipoteza hamu ya kuwa kwenye ndoa na Kardash kutokana kujihusisha na vitendo vya usaliti. “Sioni nikimuoa Prima, nilikuwa na maono hayo hapo nyuma lakini sina tena,” Geosteady alifichua. Geosteady na Prima ambao walifufua penzi lao miezi kadhaa iliyopita kwa pamoja wana watoto wawili.

Read More
 GEOSTEADY AFUNGUKA KUHUSU TAMASHA LAKE LA DINE WITH GEOSTEADY

GEOSTEADY AFUNGUKA KUHUSU TAMASHA LAKE LA DINE WITH GEOSTEADY

Msanii Geosteady ni moja kati ya wanamuziki wazuri wa Rnb kutoka Uganda. Kwa miaka mingi amekonga nyonyo za wapenzi wa mziki mzuri afrika mashariki na nyimbo kama Same way woman na nyingine nyingi. Onesho lake la kila mwaka liitwalo Dine with Geosteady ambalo lilifanya vizuri kipindi cha nyuma nchini Uganda ilisimamishwa na ujio wa janga la corona. Baada ya uchumi kufunguliwa nchini humo.wengi walidhani geosteady atatangaza tarehe ya kufanyika kwa onesho lake kama namna wasanii wengi wanavyofanya. Lakini bosi huyo Blackman Records hajaonyesha nia ya kufanya hivyo kwani amedai kuwa hana nyimbo za kutosha  kwa ajili ya kuwapa burudani mashabiki zake. “Ziko tayari kwa ajili ya onesho la muziki. Sina muziki wa kutosha”, Geosteady amesema kwenye mahojiano na Galaxy FM. Utakumbuka miongoni mwa wasanii ambao wanapanga kufanya matamasha yao ya muziki nchini uganda ni pamoja na Levixone, Chameleone, Azawi na wengine wengi.

Read More
 GEOSTEADY: “SIJAONANA NA WANANGU KWA MIAKA MITATU SASA”

GEOSTEADY: “SIJAONANA NA WANANGU KWA MIAKA MITATU SASA”

Staa wa muziki nchini uganda Geosteady amefunguka kwamba ana miaka mitatu sasa hajawatia machoni watoto wake ambao alizaa na Baby mama wake Prima Kardash. Katika mahojiano yake ya hivi karibuni Geosteady amesema baby mama wake Prima amekuwa kizingiti kwake kuwaona watoto wake ikizingitiwa  kuwa mara ya mwisho kuwaona ilikuwa mwaka wa 2022. Hitmaker huyo wa “Energy” anasema anaamini siku moja atakuja kuonana na watoto wake ila kwa sasa amehamua kuelekeza nguvu zake kwenye muziki wake ambao kwa mujibu wake utamuingiza kipato kizuri ambayo itamsaidia kuwalea watoto wake hao siku za usoni. Wawili hao waliachana miaka mitatu iliyopita wakiwa wamejaliwa watoto wawili na kila mmoja kwa sasa amesonga mbele na maisha yake kwa kuingia kwenye mahusiano mapya.

Read More