Wasanii Tanzania waonywa dhidi ya kuhamasisha dawa za kulevya kupitia nyimbo zao
Kamishna Mkuu wa Mamlaka ya Kudhibiti na Kupambana na Dawa za Kulevya, Gerald Kusaya leo jijini Dar es Salaam wakati akizungumza na waandishi wa habari ametoa onyo kwa baadhi ya wasanii wanaotunga nyimbo zenye maudhui ya kuhamasisha matumizi ya dawa za kulevya. Kusaya amesema kawa hatua kali za kisheria zitachukuliwa dhidi ya wasanii watakaokiuka agizo hilo. Hata hivyo ameongezea kwa kusema kuwa wasanii ni bora watunge nyimbo za kuhamasisha kilimo au biashara na si madawa ya kulevya kama vile bangi.
Read More