GRAND P ATEULIWA BALOZI WA UTALII NA UTAMADUNI NCHINI GUINEA

GRAND P ATEULIWA BALOZI WA UTALII NA UTAMADUNI NCHINI GUINEA

Mwanamuziki mwenye umbo dogo kutoka nchini Guinea Grand P ameteuliwa kuwa balozi wa utamaduni na utalii kuliwakilisha taifa hilo kwenye nchi jirani ya Mali Grand P kupitia ukurasa wake wa Facebook amemshukuru Kanali Mamadi Doumbuya ambaye anashikilia wadhfa wa Urais wa mpito nchini Guinea kwa kumpatia pasipoti ya kidiplomasia huku akisisitiza dhamira yake ya kufanya kazi kwa ajili ya kukuza Utamaduni wa Guinea kama kivutio cha watalii. Grand P ambaye alizaliwa mwaka 1990 huko Sanguiana, nchini Guinea, amekuwa gumzo mtandaoni kutokana na watu kuzungumzia maumbile yake yasiyo ya kawaida na gumzo hilo lilizidishwa hata zaidi baada ya kuweka wazi kuwa na mahusiano ya kimapenzi na mrembo kutoka Ivory Coast, Eudoxie Yao ambaye ni mkubwa zaidi kwa muonekano wa mwili.

Read More
 PENZI LA GRAND P NA EUDOXIE YAO LAFUFUKA TENA

PENZI LA GRAND P NA EUDOXIE YAO LAFUFUKA TENA

Kama ulikuwa unadhani penzi la Grand P na Eudoxie Yao limevunjika nikuambie tu pole. Mwanamuziki huyo mashuhuri kutoka Guinea amethibitisha kuwa bado anampenda mrembo huyo. Kupitia ukurasa wake wa Facebook Grand P ameposti mfululizo wa picha za kimahaba zaidi akiwa na Eudoxie ambapo amesisitiza kuwa ataishi kumpenda mwanadada huyo aliyebarikiwa na makalio makubwa kutoka Ivory Coast. Hivi majuzi hata hivyo, Yao alidaiwa kuachana na bilionea huyo baada ya kumuona akijiburudisha na mwanadada mwingine kwenye moja ya night club. Vyanzo vya karibu na wawili hao, vilisema mrembo huyo alihamua kubwaga manyanga baada ya kukithiri kwa tabia ya usaliti ambayo Grand P alikuwa nayo.

Read More
 GRAND P ADATA NA PENZI LA EUDOXIE YAO, ACHORA TATTOO YA JINA LAKE KWENYE KIFUNDO CHA MKONO

GRAND P ADATA NA PENZI LA EUDOXIE YAO, ACHORA TATTOO YA JINA LAKE KWENYE KIFUNDO CHA MKONO

Mwanamuziki nyota kutoka nchini Guinea Moussa Sandiana Kaba maarufu kama Grand P , ameamua kuchora tattoo yake ya kwanza katika mwili wake kwa kuandika jina la mpenzi wake mwenye umbo kubwa kumzidi, Eudoxie Yao. Grand P amechora tattoo inayosomeka ‘ 𝒍𝒐𝒗𝒆 𝒆𝒖𝒅𝒐𝒙𝒊𝒆 ‘ akionesha ni kwa namna gani anampenda mpenzi wake huyo raia wa Ivory Coast. Wawili hao walioata umaarufu zaidi mitandaonI kutokana na muonekano wa maumbo yao, ambapo Grand P yeye akiwa na ugonjwa wa kudumaa na kuonekana kuwa nA umbo dogo, huku mpenzi wake Eudoxie Yao akiwa na umbo kubwa kumzidi. Haya yanajiri ikiwa ni takribani miezi miwili kupita baada ya Grand P kumvisha Eudoxie pete ya uchumba.

Read More
 GRAND P AMVISHA PETE MPENZI WAKE EUDOXIE YAO

GRAND P AMVISHA PETE MPENZI WAKE EUDOXIE YAO

Mwanamuziki kutoka nchini Guinea, ‘Grand P’ amemvisha pete mpenzi wake wa muda mrefu Eudoxie Yao ambaye ni raia wa Ivory Coast. Wapenzi hao wawili walikuwa kwenye mahojiano na moja ya runinga nchini Gabon ambapo Grand P alipiga magoti na kumvisha Eudoxie Pete na kuahidi kutorudia makosa yaliyosababisha uhasama kati yao awali. Haya yanajiri ikiwa ni miezi kadhaa imepita tangu wawili hao watengane kutokana na tetesi za Eudoxie kwamba Grand P hakuwa mwaminifu. Mrembo Eudoxie Yao alitangaza kuachana na Grand P, Julai mwaka 2021 baada ya picha za Grand P akimbusu mwanamke mwingine kusambaa mitandaoni.

Read More
 PENZI LA MWANAMUZIKI GRAND P NA EUDOXIE YAO LAFUFUKA TENA

PENZI LA MWANAMUZIKI GRAND P NA EUDOXIE YAO LAFUFUKA TENA

Mwanamuziki mashuhuri kutoka Guinea Moussa Sandiana Kaba almaarufu Grand P amethibitisha kuwa bado anampenda soshalaiti Eudoxie Yao miezi kadhaa baada ya ripoti kuenea kuwa wametengana. Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Grand P amesema ataishi kumpenda mwanadada huyo aliyebarikiwa na makalio makubwa kutoka Ivory Coast ambapo amedhihirisha upendo wake kwake usio na mwisho. “Wewe na mimi ni wa maisha. Shukran” Grand P alimwandikia Yao. Kauli ya Grand P imekuja siku chache baada Eudoxie Yao kumtaja bilionea huyo kama Ex wake baada ya kumuona akijiburudisha na wanadada wengine ndani ya bwawa la kuogelea. Utakumbuka takriban miezi miwili iliyopita Grand P alidai kupokonywa mchumba wake Eudoxie Yao baada ya picha za mrembo huyo na mwanamuziki kutoka Congo Roga Roga kusambaa mitandaoni wakiwa wanajiburudisha, jambo ambalo lilimtia Grand P hofu kuwa huenda  Roga Roga alikuwa na nia ya kumpokonya mpenzi wake huyo. Hata hivyo Grand P ambaye ana maumbile ya kipekee alimpa onyo kali Roga Roga dhidi ya kuendeleza mahusiano na mkewe. “Ndugu yangu Roga Roga nakuheshimu sana wewe na watu wote wa Kongo… Lakini  njia unayotaka kufuata si ya kupendeza, usifurahie kuwa karibu na mke wangu la sivyo nitachukua hatua mbaya. Hii ni onyo, Asante!” Grand P aliandika kwenye mtandao wa Facebook.

Read More
 EUDOXIE YAO BADO ANA MAPENZI KWA EX WAKE GRAND P, AMTAKIA KHERI KWENYE MAISHA YAKE MAPYA

EUDOXIE YAO BADO ANA MAPENZI KWA EX WAKE GRAND P, AMTAKIA KHERI KWENYE MAISHA YAKE MAPYA

Mwanamitindo mwenye shepu matata kutoka nchini Ivory Coast Eudoxie Yao amemtakia kila la kheri katika maisha aliyekuwa mpenzi wake Grand P, baada ya kumuona kwenye video akijivinjari katika bwawa la kuogelea na mwanamke mwingine. Katika video hiyo, mwanamuziki huyo kutoka Guinea mwenye umbile dogo zaidi ameposti video Facebook akiwa amejiachia na mrembo wake mpya. “Maisha ni kitu cha kuvutia sana, jibambe kadri ya uwezo wako. Mimi najivinjari kivyangu,” aliandika Grand P Katika comment aliyekuwa mpenzi wake, Eudoxie Yao ameandika ujumbe wa kumtakia kila la kheri katika Maisha. Fununu za kuachana kwa wawili hao zilizuka wakati wa mashindano ya AFCON nchini Cameroon mapema mwezi Februari wakati mwanaume huyo mdogo alipoonekana akiwa na wanawake wengi jambo linalotajwa kumkera Eudoxie na kumpelekea kufanya maamuzi ya kumuacha Grand P.

Read More