GRENADE AJIUNGA NA LEBO YA MUZIKI YA TEAM NO SLEEP

GRENADE AJIUNGA NA LEBO YA MUZIKI YA TEAM NO SLEEP

Miaka mitatu iliyopita bosi wa Team No Sleep alimsaini msanii Grenade kwenye lebo yake na wasanii kama Sheebah na Roden Y Kabako. Jeff Kiwa na Grenade waliingia kwenye ugomvi na wakavunja uhusiano wao baada ya msanii huyo kususia show yake mashariki mwa Uganda. Jambo hilo lilimfanya Grenade kujiunga na lebo nyingine ya muziki iitwayo Rydim empire inayomilikiwa na Derrick Orone. Wawili hao hawakufanikiwa kufanya kazi pamoja kama walivyoahidiana ambapo grenade alienda mbali zaidi na kuanza kufanya kazi na meneja wa lebo ya muziki aitwaye  peterson. Sasa taarifa mpya ni kuwa Jrff kiwa amemsainisha tena Grenade ndani ya lebo yake ya muziki ya Team No Sleep. Hata hivyo Grenade amethibitisha taarifa hiyo na kusema kwamba anaamini Jeff Kiwa atamsaidia kuupeleka muziki wake kwenye kiwango kingine.

Read More
 GRENADE AFUNGUKA JUU YA KUTOKA KIMAPENZI NA WANAWAKE WAZEE

GRENADE AFUNGUKA JUU YA KUTOKA KIMAPENZI NA WANAWAKE WAZEE

Mwanamuziki kutoka Uganda Grenade amefunguka kuhusu madai ya kuwa kwenye mahusiano ya kimapenzi na wanawake waliomzidi umri. Katika mahijiano yake hivi karibuni Grenade amesema licha ya changamoto alizokutana nazo akiwa anawachumbia, hajutii kutoka kimapenzi na wanawake wazee kwa kuwa yeye ni mtu mzima ambaye anafanya maamuzi yake binafsi. Kauli ya imekuja siku chache baada ya aliyekuwa mpenzi wake Kilooto kumfungulia mashtaka mahakamani kwa madai ya kuingia kwake bila idhini ambapo kesi yake itasikilizwa Juni 28 mwaka huu.

Read More
 GRENADE AACHIWA HURU KWA DHAMANA

GRENADE AACHIWA HURU KWA DHAMANA

Mwanamuziki kutoka nchini Uganda Grenade ameachiwa uhuru kutoka jela ikiwa ni siku chache tangu kukamatwa kwake. Grenade alitiwa mbaroni na polisi nchini humo kwa tuhuma za kumzaba makofi aliyekuwa mpenzi wake Kilooto baada ya uhusiano wao wa kimapenzi kuingiwa na ukungu miezi kadhaa iliyopita. Juni mosi mwaka huu Grenade alifikishwa mahakamani ambapo alikana madai ya kumpiga na kumjeruhi mpenzi wake wa zamani Kilooto mbele ya Hakimu mkazi wa Kajjansi. Hata hivyo aliachiwa huru kwa dhamana huku akionywa kutorudia kosa la kumshambulia mpenzi wake tena. Kesi ya Grenade itasikilizwa kwa mara ya pili Juni 29 mwaka huu na kama akikutwa na hatia ya kosa hilo, huenda akahukumiwa kifungo cha miaka 2 gerezani. Utakumbuka baada ya uhusiano wa Grenade na Ex wake Kilooto kuvunjika mrembo huyo alimuanika hadharani kuwa amekuwa akimsaliti kimapenzi na kujihusisha na vitendo vya kishirikina kwa ajili ya kumshawishi azidi kumuonyesha upendo.

Read More
 GRENADE AFUNGUKA SABABU ZA WAREMBO WA UGANDA KUMGANDA KAMA GUNDI

GRENADE AFUNGUKA SABABU ZA WAREMBO WA UGANDA KUMGANDA KAMA GUNDI

Msanii kutoka nchini Uganda Grenade amefunguka siri ambayo imewafanya wanawake wengi nchini humo kumpenda bila sababu za msingi. Kwenye mahojiano na Galaxy FM Grenade amejitapa kuwa ana ujuzi wa kipekee linapokuja swala la kutumia ulimi wake kuwashawishi wanawake ambapo ameenda mbali zaidi na kujinasibu kuwa swala hilo limewafanya wanawake wengi nchini uganda kumzimia kimapenzi. Grenade amekuwa akihusishwa kutoka kimapenzi na wanawake wengi nchini uganda akiwemo  Lydia Jazmine, Vivian Mbuga, Sheila Gashumba, Zari na wengine wengi. Hata hivyo mbinu anazozitumia  Grenade kuwavutia warembo hao limeilkuwa kitendawili kwa  waganda wengi lakini Good news kuwa msanii huyo amenyoosha maelezo kuhusu hilo

Read More