Guardian Angel: Natumia Milioni 1.5 Kila Mwezi!

Guardian Angel: Natumia Milioni 1.5 Kila Mwezi!

Msanii wa muziki wa injili nchini Kenya, Guardian Angel, amefichua kiwango kikubwa cha fedha anachotumia kila mwezi kugharamia mahitaji yake ya msingi. Akipiga stori na podcast ya Mwakideu live, Guardian Angel amesema kuwa matumizi yake ya kila mwezi ni zaidi ya Shillingi milioni 1.5. Kwa mujibu wa msanii huyo, kiasi hicho kinahusisha gharama za maisha, miradi ya muziki, pamoja na majukumu mengine ya kifamilia na kijamii anayobeba. Amebainisha kuwa licha ya muziki wa injili kutoonekana kama sekta yenye mapato makubwa, yeye ameweza kujipanga kimaisha kuhakikisha anadumisha kiwango chake cha maisha. Kauli yake imezua mjadala mitandaoni, baadhi ya mashabiki wakisifia uaminifu na uthubutu wake wa kuweka wazi hali yake ya kifedha, huku wengine wakishangazwa na ukubwa wa gharama hizo.

Read More
 Guardian Angel athibitisha mapenzi hayachagui umri, ampongeza mkewe kwa maneno ya kutia moyo

Guardian Angel athibitisha mapenzi hayachagui umri, ampongeza mkewe kwa maneno ya kutia moyo

Msanii maarufu wa nyimbo za Injili nchini Kenya, Guardian Angel, amemiminia mkewe, Esther Musalia, ujumbe mtamu wa mapenzi huku akimsherehekea kwenye siku yake ya kuzaliwa ya kutimiza miaka 55. Kupitia mitandao ya kijamii, Guardian Angel aliandika ujumbe wenye hisia kali akimtaja Esther kama baraka kubwa katika maisha yake. “Kukupenda kulikuwa uamuzi bora zaidi wa maisha yangu. Namshukuru Mungu kila siku kwa kunibariki kwa kukupa wewe. Heri ya siku ya kuzaliwa, malkia wangu,” aliandika Guardian Angel kwenye ukurasa wake wa Instagram, akiambatanisha na picha wakiwa pamoja kwa furaha. Wawili hao wamekuwa kwenye uhusiano wa karibu na wa kudumu, licha ya tofauti kubwa ya umri kati yao, na wamekuwa wakivutia wengi kwa jinsi wanavyopendana na kushikilia ndoa yao kwa imani thabiti. Mashabiki na wafuasi wao wamejitokeza kwa wingi mtandaoni kuwatakia heri, huku wengi wakimsifu Guardian kwa kumuenzi mkewe hadharani na kuvunja mitazamo ya kijamii kuhusu ndoa zenye tofauti kubwa ya umri. Guardian Angel, anayejulikana kwa nyimbo maarufu kama Nadeka, Swadakta na Uskonde, ameendelea kuwa miongoni mwa wasanii wa Injili wanaoheshimika zaidi katika ukanda wa Afrika Mashariki, si tu kwa kipaji chake, bali pia kwa misimamo yake kuhusu ndoa, imani na familia.

Read More
 Guardian Angel ataka kanisa kuunga mkono wasanii wa nyimbo za injili

Guardian Angel ataka kanisa kuunga mkono wasanii wa nyimbo za injili

Mwimbaji wa nyimbo za injili kutoka Kenya Guardian Angel ametoa changamoto kwa makanisa kuanza kuunga mkono kazi za wasanii wa nyimbo za injili nchini humo. Kupitia ukurasa wa Instagram amesema wasanii wengi huenda wakaacha kujihusisha na muziki huo kabla mwaka 2023 haujaisha na kugeukia muziki wa kidunia kama hawatapata uungwaji mkono kutoka kwa wakristo. Hata hivyo amesisitiza kuwa iwapo makanisa yataitikia wito huo hakuna msanii wa nyimbo za injili ataacha muziki huo kwa kuwa wengi wao wanatapitia mazingira magumu kwenye masuala ya kuingiza riziki kupitia muziki wao. “2023 THE CHURCH MUST BEGIN TO SUPPORT KENYAN GOSPEL MUSICIANS…Otherwise things will be tough. Most of them might close down before the End of the Year:” “Hakuna msanii wa GOSPEL ataacha gospel tena sababu anaimba akiteseka….Choose what to do with This information”, Aliandika.

Read More
 Guardian Angel aachia rasmi album yake mpya “Arise and Shine”

Guardian Angel aachia rasmi album yake mpya “Arise and Shine”

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini  Guardian Angel ameachia rasmi album yake mpya inayokwenda kwa jina la  Arise and Shine. Victory imebeba jumla ya mikwaju 10 ya moto huku  ikiwa na kolabo 3 pekee kutoka kwa wasanii kama Miracle, DJ Kezz na Kamuhunjia. Album hiyo ambayo ndio kazi ya mwisho ya Guardian Angel kwa mwaka 2022, inapatikana ‘Exclusive’ kupitia mitandao yote ya  kukisikiliza na kuuza muziki duniani kama vile Boomplay,Spotify na Apple Music Album ya ” A rise and Shine ” ni album ya tatu kwa mtu mzima  Guardian Angel  tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Victory na Thanks for Coming zilizotoka mwaka 2021.

Read More
 ESTHER MUSILA ATOA WITO KWA WANAWAKE KUWAWEKA WAUME ZAO KWA MAOMBI

ESTHER MUSILA ATOA WITO KWA WANAWAKE KUWAWEKA WAUME ZAO KWA MAOMBI

Mke wa msanii Guardian Angel,Esther Musila ametoa changamoto kwa wanawake walio kwenye ndoa kujenga tabia ya kuwaweka waume zao kwenye maombi. Akipiga stori na SPM BUZZ Musila amesema maombi yana nguvu kubwa sana katika maisha ya ndoa kwa kuwa inaleta familia pamoja lakini pia inawasaidia wanandoa kufanikisha baadhi ya mipango yao. Mwanamama huyo wa miaka 52 amesema amekoshwa sana na mienendo ya mama taifa Bi Rachel Ruto ya kumtanguliza Mungu kwa kila jambo ambapo amehapa kwamba atafuata nyayo zake kuhakikisha mume wake Guardian Angel anafanikisha ndoto zake katika maisha. Utakumbuka Guardian Angel na mke wake Esther Musila ni miongoni mwa wasanii watakao toa burudani Septemba 13 katika hafla ya kuapishwa kwa Rais mteule wa Kenya Dkt. William Samoe Ruto kwenye uga wa kamataifa wa Kasarani.

Read More
 GUARDIAN ANGEL AWAJIBU WANAODAI MUZIKI WA INJILI HAUNA PESA

GUARDIAN ANGEL AWAJIBU WANAODAI MUZIKI WA INJILI HAUNA PESA

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Guardian Angel amewatolea uvivu wanaodai kuwa wasanii wa gospel wamefulia kiuchumi. Katika mahojiano yake hivi karibuni Guardian Angel amesema madai ya kuwa muziki wa injili hauna pesa hayana ukweli wowote ambapo ameenda mbali zaidi na kusema kuwa yeye ni moja kati ya wasanii ambao wana mkwanja mrefu  na hata ikitokea ameacha muziki pesa zake zitamsaidia kujikimu kimaisha. Katika hatua nyinngine amepinga madai kuwa Ringtone ameacha muziki wa injili kwa kusema kwamba haamini kabisa kama msanii huyo amekimbilia muziki wa kidunia kwani huenda anatumia jambo hilo kutengeneza mazingira ya kuzungumzia. Guardian Angel ametoa kauli hiyo baada ya walimwengu kuhoji kuwa tasnia ya muziki nchini kenya haina pesa na ndio maana wasanii wengi waliokuwa wanafanya muziki huo wamegeukia muziki wa kidunia.

Read More
 GUARDIAN ANGEL AKANUSHA KULELEWA NA ESTHER MUSILA

GUARDIAN ANGEL AKANUSHA KULELEWA NA ESTHER MUSILA

Mwimbaji wa nyimbo za injili nchini Guardian Angel amekanusha madai yanayosambaa mtandaoni kuwa amekuwa akilelewa na mke wake Esther Musila. Katika mahojiano yake hivi karibuni Guardian Angel amenyosha maelezo kwa kusema kwamba madai hayo hayana msingi wowote kwa kuwa yeye ndiye huwa anagharamia mahitaji yote ya msingi kwa mke wake kama mume. “Hajawai kulipa bills za nyumba yangu kwa sababu mimi ndo bwana yake, mimi ndo nalipa bills zake. Na pia kama kuwekwa ni namna hiyo basi mimi sielewi. Na kama mtu anahisi hio ndo kuwekwa basi iko tu sawa. Si mimi ndo nawekwa, wewe unawashiwa nini,” Amesema. Hitmaker huyo wa Nadeka ameenda mbali zaidi na kusema kuwa kama kufurahia ndoa na kupendwa ndio imewaaminisha watu kuwa analelewa na mke wake Esther Musila, basi yupo radhi kufanya hivyo. “Kama hivi ndo kuwekwa inaonjaacha niwekwe milele wacha niwekwe zaidi, ni tamu. Because kama nimewekwa hata sifai kupost anything ya the lady I’m purported to be with. I have never said that she is my sugar mummy secondly, I have never lived in her house, it is her who came to my house, kwa hiyo mimi ndo mzee wa hiyo nyumba.” Amesisitiza Guardian Angel.

Read More
 GUARDIAN ANGEL AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA CHINI YA SEVEN HEAVEN MUSIC

GUARDIAN ANGEL AMTAMBULISHA MSANII WAKE MPYA CHINI YA SEVEN HEAVEN MUSIC

Nyota wa muziki nchini Guardian Angel amemtambulisha rasmi msanii mpya ndani ya lebo yake ya muziki ya Seven Heaven Music. Katika mahojiano yake hivi karibuni Guardian Angel amesema msanii huyo kwa jina la DJ Kezz kenya atakuwa chini ya lebo ya  Seven Heaven Music  ambayo itasimamia kazi zake zote za muziki ambapo amewataka mashabiki zake wamkaribishe msanii huyo kwenye tasnia ya muziki nchini Hitmaker huyo wa ngoma ya “Deka” amesema ametumia kiasi cha shillingi milllioni 6 kutambulisha msanii huyo kwa mashabiki ikiwemo kutayarisha video za nyimbo zake tatu ambazo zitatoka karibuni. Kwa upande wake DJ Kezz kenya ambaye ni msanii wa kwanza kujiunga na lebo ya Seven Heaven Music, ameonyesha furaha yake kujiunga na familia ya  Seven Heaven Music kwa kusema kwamba  mashabiki wakae mkao wa kula kupokea nyimbo zake. Utakumbukwa kwa sasa  DJ Kezz kenya anafanya vizuri na wimbo wake mpya uitwao Jipende aliyomshirikisha bosi wake Guardian Angel ambao una zaidi ya views laki moja kwenye mtandao wa youtube ndani ya siku 4 tangu iachiwe rasmi.

Read More
 GUARDIAN ANGEL AZINDUA JUKWAA LAKE LA KUSTREAM VIDEO ZA MUZIKI

GUARDIAN ANGEL AZINDUA JUKWAA LAKE LA KUSTREAM VIDEO ZA MUZIKI

Mwanamuziki wa nyimbo za injili Guardian Angel na mke wake Esther musila wamezindua jukwaa lao la kustream video za muziki Jukwaa hilo liitwalo Solution.co.ke litatoa fursa kwa wasanii wa kenya na watengeneza maudhui kuingiza kipato kupitia maudhui wanayopakia kupitia mtandao kwa gharamu nafuu sana tofauti na majukwaa mengine kama Youtube Hata hivyo Guardian Angel amesema hivi karibuni atatoa muongozo wa namna ambavyo wanamuziki na wabunifu watakavyowasilisha kazi zao kwenye mtandao. Tayari couple hiyo imepakia video ya harusi yao na video ya wimbo mpya wa Guardian Angel uitwao money kwenye mtandao huo.

Read More
 GUARDIAN ANGEL AMVUA NGUO ANDREW KIBE KWA KUIKOSOA NDOA YAKE NA ESTHER MUSILA, AMUITA JINI SHETANI

GUARDIAN ANGEL AMVUA NGUO ANDREW KIBE KWA KUIKOSOA NDOA YAKE NA ESTHER MUSILA, AMUITA JINI SHETANI

Msanii wa nyimbo za injili nchini Guardian Angel amemtolea uvivu mwanahabari mwenye utata Andrew Kibe kwa madai ya kuikosoa ndoa yake na mke wake Esther Musila. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Guardian Angel amemtaka kibe aheshimu maamuzi yake na mke wake Esther Musila kuhalilisha ndoa kwa njia ya harusi ikizingatiwa kuwa wao ni watu wazima ambao upendo uliwaleta pamoja licha ya utofauti wa umri wao. “Maandiko matakatifu yanasema wakati mtu ameokoka aki-backslide, nini umu-happenia?…huwa anakuwa hatari zaidi kwani huwa anaingiliwa na shetani mara saba. Sina muda wa kupishana na shetani, vita vyetu ni vya kiroho my friend”..amesema kwenye mahojiano na Plug TV. Hitmaker huyo wa “Nadeka” ameenda mbali na kumshauri Kibe akome kuingilia maisha yao na badala yake aelekeze nguvu zake kwenye shughuli zitakazomuingizia kipato kwani anapoteza muda wake kuzungumzia jambo ambalo litamsaidia maishani. Kauli ya Guardian Angel imekuja mara baada ya Andrew Kibe kuonekana kukejeli ndoa yake na mke wake Esther Musila kwa kusema kwamba haoni ndoa hiyo ikidumu kwani msanii huyo aliwavunjia heshima vijana wa Kenya kwa hatua kumuoa mwanamke aliyemzidi kiumri.

Read More
 ALBUM YA GUARDIAN ANGEL “VICTORY” YAWEKA REKODI BOOMPLAY

ALBUM YA GUARDIAN ANGEL “VICTORY” YAWEKA REKODI BOOMPLAY

Mwanamuziki wa nyimbo za injili nchini Guardian Angel anazidi kufanya vizuri kupitia mauzo ya mtandaoni na Album yake ” Victory ” ambayo tayari ina takriban miezi miwili tangu itoke rasmi. Goods ni kwamba Album ya “Victory”  imefanikiwa kufikisha jumla ya Streams millioni moja kwenye mtandao wa kusikiliza na kupakua muziki wa Boomplay Kenya. Album ya “Victory” iliachiwa rasmi Novemba 11 mwaka 2021 ikiwa na jumla ya ngoma 10 ya moto na ni album ya pili kwa mtu mzima  guardian angel  tangu aanze safari yake ya muziki baada ya Thanks for Coming iliyotoka mwezi mei mwaka 2021  

Read More
 GUARDIAN ANGEL AFUNGA NDOA YA SIRI NA MCHUMBA WAKE ESTHER MUSILA

GUARDIAN ANGEL AFUNGA NDOA YA SIRI NA MCHUMBA WAKE ESTHER MUSILA

Nyota wa muziki wa injili nchini Guardian Angel ameripotiwa kufunga ndoa ya siri na mchumba wake Esther Musila  baada ya kuwa kwenye mahusiano kwa takribani mwaka mmoja. Kulingana na wajuzi mambo kwenye mitandao ya kijamii,Harusi hiyo ambayo inadaiwa kuwa ya siri imiefanyika leo jijini Nairobi na kuhudhuriwa na wageni wasiozidi 20, ikiwemo ndugu wa pande zote mbili za familia zao. Hata hivyo mashabiki wengi kwenye mitandao ya kijamiii wamefurahia kwa hatua ya wawili hao kuhalalisha mahusiano yao huku wengine wakiwa na mshangao kwanini ndoa hiyo imekuwa ya siri japokuwa ni jambo la kheri kwa kila mwanadamu Uhusiano wa kimapenzi wa hao ulianza mapema mwaka jana 2021, huku Guardian Angel akithibitisha mahusiano hayo rasmi baada ya ukaribu wake na mwanamama huyo mwenye umri wa miaka 51 gumzo mtandaoni ambapo  wengi walishangazwa na hatua ya msanii huyo kutoka kimapenzi na mtu ambaye amemzidi umri.

Read More