Mwanamuziki wa Bongofleva H. Baba amtolea uvivu Harmonize kwa kumuiga Wizkid

Mwanamuziki wa Bongofleva H. Baba amtolea uvivu Harmonize kwa kumuiga Wizkid

Msanii wa Bongofleva H. Baba amedai kitendo cha Harmonize kumchagua Kajala kuwa Meneja wake ni matokeo ya kumuiga Wizkid ambaye mke wake, Jada P ndiye Meneja wake. H. Baba amesema Meneja na mahusiano ni vitu viwili tofauti, huwezi kuvichanganya na kupata matokeo mazuri na pengine ndio sababu ya baadhi ya wasanii kuondoka Konde Music. “Wanataka kuiga kwa Wizkid, hawawezi. Meneja au mke wa Wizkid alikuwa anamsimamia Chris Brown, kwa hiyo kuja kumsimamia Wizkid ni jambo jepesi kwa sababu ana uzoefu, sasa huyu dada yetu hana uzoefu wa hicho” amesema H. Baba. Utakumbuka tangu Kajala Masanja amekuwa Meneja wa Konde Music, wasanii watatu, Cheed, Killy na Anjella wameachana na lebo hiyo.

Read More
 H. BABA AMWAGIA SIFA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KULAMBA UBALOZI WASAFI BET

H. BABA AMWAGIA SIFA DIAMOND PLATNUMZ BAADA YA KULAMBA UBALOZI WASAFI BET

Mwanamuziki wa Bongofleva H.Baba ameweka wazi kulipwa kiasi kikubwa cha fedha na Diamond Platnumz kuwa balozi wa kampuni yake ya michezo ya kubashiri ya wasafi bet. Baba, ametumia Instagram page yake kutoa pongezi na shukrani kwa msanii huyo na uongozi mzima wa WCB, ambao awali alionekana kuwarushia maneno makali mtandaoni kwa ajili ya kumsapoti mwanamuziki Harmonize. Katika hatua nyinngine H. Baba ameweka wazi kuhusu kumuandalia Diamond Platnumz tuzo yake binafsi kama ambavyo amekuwa akifanya kwa Harmonize. H.Baba ametangaza kuwa shabiki rasmi wa WCB Wasafi huku akiwaomba radhi mashabiki wa lebo hiyo.

Read More
 H.BABA AKATA TAMAA KUDAI HAKI YAKE KUTOKA KWA HARMONIZE

H.BABA AKATA TAMAA KUDAI HAKI YAKE KUTOKA KWA HARMONIZE

Mwanamuziki wa Bongofleva H.Baba amefunguka kuhusu madai ya kutofaidi na mirabaha ya wimbo wa Attitude aliyoshirikishwa na Harmonize. Kuptia ukurasa wake wa Instagram H.Baba amesema ameamua kumuachia Mungu suala hilo na kwa sasa amerudi kwenye maisha yake ambayo hadhulumiwi. “Kila chenye mwanzo kina mwisho mdogo wangu, haya yote yatakurudia tu, utadhulumika na wewe na utalalamika kama ulivyolalamika pale Airport, ila jasho langu mimi Mungu atanilipia” – Ameandika H.Baba. H.Baba amefunguka hayo baada ya kudai kudhulumiwa jasho lake kutokana na ushiriki wake katika wimbo wa Attitude ambao alidai kuwa hakupata chochote katika pande zote mbili yaani audio na video ambapo alienda mbali na kumtaka Harmonize amlipe

Read More
 H. BABA AMJIA JUU HARMONIZE KISA MIRAHABA YA WIMBO WA ATTITUDE

H. BABA AMJIA JUU HARMONIZE KISA MIRAHABA YA WIMBO WA ATTITUDE

Mwanamuziki wa bongofleva, H. Baba ameibuka kudai haki yake kutoka kwa Harmonize ambaye wamewahi kufanya nae kazi ya ushirikiano kupitia wimbo wa “Attitude” ambao ulitoka Aprili 23, mwaka jana akiwemo pia gwiji kutoka DR Congo, Awilo Longomba. Kupitia ukurasa wake wa instagram, H. Baba amedai kudhulumiwa jasho lake kutokana na ushiriki wake katika wimbo huo kwa kutoambulia chochote katika pande zote mbili yaani audio na video ambapo amemsihi kwamba Harmonize amlipe. “Nakuheshimu sana, usidhulumu jasho langu mdogo wangu” inasomeka sehemu ya ujumbe wa H.Baba aliouandika kwenye ukurasa wake wa Instagram. Wimbo “Attitude” ni moja kati nyimbo kutoka kwa Harmonize iliyopata mafanikio makubwa, hadi sasa video ya wimbo huo ina views Milioni 15 katika mtandao wa youtube huku Boomplay ikiwa na streams Milioni 2.1

Read More
 H. BABA AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMU-UNFOLLOW HARMONIZE NA KUMFUATA DIAMOND PLATINUMZ INSTAGRAM

H. BABA AZUA GUMZO MTANDAONI BAADA YA KUMU-UNFOLLOW HARMONIZE NA KUMFUATA DIAMOND PLATINUMZ INSTAGRAM

Mwanamuziki wa Bongofleva, H. Baba kwa sasa anam-follow Diamond Platnumz pekee kwenye ukurasa wake wa Instagram ambao una followers zaidi ya laki 6. Juzi kati H. Baba alimpongeza Diamond kwa kutumbuiza kwenye show maalumu iliyoandaliwa na waandaaji wa tuzo za Grammy, Recording Academy iitawayo Global Spin ambayo ina lengo la kuuibua na kuutangaza zaidi muziki wa Afro Beat, Pop na Latin Music. Hatua hiyo iliwashangaza wengi kwani kwa miaka ya hivi karibuni H. Baba alikuwa karibu sana na Harmonize hadi kushirikiana kwenye wimbo, uitwao Attitude ambao Awilo Longomba kutoka DRC Congo naye alishirikishwa. Kwa inavyoonekana sasa uhusiano kati ya H. Baba na Harmonoze umeingia na ukungu baada ya kuamua kumu-unfollow Instagram na kum-follow Diamond pamoja na kuupigia debe muziki wake.

Read More