HAMISA MOBETTO ALAMBA DILI NONO LA UBALOZI WA VIPODOZI VYA WHITENICIOUS

HAMISA MOBETTO ALAMBA DILI NONO LA UBALOZI WA VIPODOZI VYA WHITENICIOUS

Mwanamuziki na mwanamitindo kutoka Tanzania Hamisa Mobetto amelamba dili nono la ubalozi wa vipodozi vya White nicious kwa upande wa Bara la Afrika akimsaidia mwanadada Blac Chyna ambaye ni Balozi wa bidhaa hizo. Mobetto ametangazwa rasmi Machi 2, mwaka wa 2022 kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa bidhaa hizo za asili zenye uwezo wa kupendezesha ngozi bila ya madhara. Akithibitisha hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram, Mobetto amesema vipodozi hivyo vya asili havina kemikali inayoharibu ngozi na kwamba vimethibitishwa na mamlaka husika kutumika kwa wanaume na wanawake. Lakini Pia ametaja bidhaa hizo ni kongwe sokoni zikiwa na miaka 30. Hata hivyo inaonekana Milango ya kibiashara inazidi kufunguka kwa mwanamitindo huyo kwani ukiachilia mbali kuwa balozi wa bidhaa hizi za urembo za kimataifa pia ni balozi wa kinywaji cha kishua cha Belaire

Read More
 HAMISA MOBETO AKANA KUWA KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA RAPPER RICK ROSS KUTOKA MAREKANI

HAMISA MOBETO AKANA KUWA KWENYE MAHUSIANO YA KIMAPENZI NA RAPPER RICK ROSS KUTOKA MAREKANI

Mrembo na msanii wa Tanzania Hamisa Mobetto amekana madai kwamba yupo kwenye uhusiano wa kimapenzi na Rapa wa Marekani Rick Ross. Akizungumza katika mahojiano na runinga ya NTV, Msanii huyo ambaye pia ni mfanyabishara amethibitisha kwamba yeye ni rafiki wa karibu wa rapa huyo wa Marekani. Wawili hao wamekuwa wakihusishwa kuwa ni couple mara baada ya Novemba 25, mwaka wa 2021 kuonekana wakiwa Dubai wakila bata pamoja. Kubwa zaidi walionekana wakicheza muziki kwenye moja ya kumbi za starehe kwa kukumbatiana kimahaba.

Read More
 HAMISA MOBETTO AWEKA WAZI MAMBO YALIYOMDATISHA KWA RAPA RICK ROSS

HAMISA MOBETTO AWEKA WAZI MAMBO YALIYOMDATISHA KWA RAPA RICK ROSS

Kama ulikuwa unadhani ni fedha na umaarufu alionao rapper kutoka marekani Rick Ross ndio vitu pekee viivyo m’datisha mrembo mtanzania Hamisa Mobetto kiasi cha kuwa nae karibu basi haya ndio majibu rasmi kutoka kwa mwanadada huyo. Akijibu swali la moja ya shabiki alietaka kujua ni kitu gani kiimfanya ampende rapper huyo raia wa marekani n mmiliki wa record label ya Maybach Music , Hamisa alimjibu kwa kuorodhesha vitu hivyo kuwa ni ndevu zake, rangi, meno na sauti yake huku akimwagia sifa lukuki kwamba rapper huyo ananukia vizuri. Ikumbukwe Hamisa Mobetto amekuwa akihusishwa kuwa penzini na msanii kutoka Marekani Rick Ross, baada wawili hao kuonekana wakiwa pamoja Novemba 25, mwaka 2021 katika falme za kiarabu Dubai wakila bata pamoja.

Read More