HAMISA MOBETTO AKANUSHA KUMFICHA MPENZI KWA HOFU YA KUPOKONYWA

HAMISA MOBETTO AKANUSHA KUMFICHA MPENZI KWA HOFU YA KUPOKONYWA

Mwimbaji na Mwanamitindo maarufu Tanzania, Hamisa Mobetto amekanusha madai kuwa amekuwa akimficha mpenzi wake wa sasa kwa kuhofia kupokonywa. Akizungumza na Wanahabari siku ya jana, Mobetto alieleza kuwa kwa kawaida huwa hathamini kuyaanika mahusiano yake hadharani. “Mimi naamini kama kitu ni chako na Mungu amepanga, basi kitakufikia na hakitakuwa cha kuibiwa. Siamini kama mwanaume anaweza kuibiwa” amesema. “Sio kama namficha, mimi na yeye tuko vizuri katika mapenzi yetu. Tunakula, tunatembea pamoja, yaani tuko vizuri,” alisema Hamisa. Pia alidai kuwa sio sawa kwake kuendelea kuwatambulisha wapenzi wapya kila wanapokuja katika maisha yake. “Tukifika mbele huko kama Mwenyezi Mungu alimuandikia kuwa mume wangu basi huenda watu wataanza kumjua. Lakini sasa hivi kama tukiachana? nikipata mwingine tena nimtambulishe,” alisema. Aidha, alibainisha kuwa kuweka mahusiano hadharani mara nyingi huwafanya watu waache kujizingatia na badala yake kuzingatia penzi.

Read More
 HAMISA MOBETTO KUNUNUA PRIVATE JET

HAMISA MOBETTO KUNUNUA PRIVATE JET

Baada ya kuzawadiwa Range Rover na mpenzi wake, Mwanamitindo na Msanii wa Bongofleva, Hamisa Mobetto ameweka wazi kiu yake ya kununua private Jet. Hamisa ameweka wazi hilo kupitia ukurasa wake wa Instagram ambapo alikuwa anashukuru kwa kupata gari hilo alilokabidhiwa wikiendi iliyopita. “Mungu hakupi unachotaka, anakupa unachostahili,” alisema Hamisa katika ujumbe wake. Endapo Hamisa akifanikisha hilo, ataungana na wasanii wa Afrika wenye Private Jet kama Davido, Cassper Nyoves, P Square, DJ Cuppy, Wizkid na wengineo.

Read More
 HAMISA MOBETTO AACHIA RASMI YOURS TRULY EP

HAMISA MOBETTO AACHIA RASMI YOURS TRULY EP

Msanii wa Bongofleva Hamisa Mobeto ameachia rasmi EP yake mpya iliyokuwa ikisubiriwa kwa hamu na mashabiki zake. EP hiyo inakwenda kwa jina la Yours Truly ina jumla ya nyimbo 4 na bonus track moja ambapo amewashirikisha wakali kama Otile Brown na Korede Bello. Kupitia ukurasa wake rasmi wa Instagram Hamisa Mobetto ameshare artwork pamoja na Tracklist ya EP hiyo ambayo ina nyimbo kama  Wewe, Want, Murua, Yanini na Pop It. Yours Truly ni EP ya kwanza kwa mtu mzima Hamisa Mobetto tangu aanze safari yake ya muziki  na inapatikana exclusive kupitia mtandao wa kupakua na kusikiliza muziki wa BoomPlay.

Read More
 HAMISA MOBETTO MBIONI KUACHIA EP YAKE MPYA

HAMISA MOBETTO MBIONI KUACHIA EP YAKE MPYA

Mwimbaji wa Bongofleva, Hamisa Mobetto amethibitisha kuachia Extended Playlist (EP) yake mpya wiki hii. Hamisa amebainisha hayo akizungumza na waandishi wa habari alipokuwa akitangaza kupata dili nono la ubalozi wa Kampuni ya “House of beauty” “Wiki ijayo natoa EP yangu, itakuwa ni ya kwanza tangia nimeanza safari yangu ya muziki, tulikuwa tunabishana kati ya kutoa albamu au tutoe EP, kwa hiyo naona jambo limekimbilia kwenye EP” amesema Hamisa. Mbali na muziki, milango ya kibiashara inazidi kufunguka kwa mwanamitindo huyo kwani ukiachilia mbali kuwa balozi wa bidhaa za urembo pia ni balozi wa kinywaji cha kishua cha Belaire.

Read More