WASANII HANSON BALIRUNO NA HALIMA NAMAKULA KWENYE KASHFA YA WIZI

WASANII HANSON BALIRUNO NA HALIMA NAMAKULA KWENYE KASHFA YA WIZI

Wasanii Halima Namakula and Hanson Baliruno wameingia kwenye headlines nchini Uganda mara baada ya kutuhumiwa kumtapeli promota wa muziki nchini humo Eddies K Promotions shillling laki 2 za Kenya. Kulingana na Eddie K Promotions, Halima Namakula na Hanson Baliruno walimuibia pesa hizo baada ya performance yao huko Mubunde nchini Uganda ambapo waliwatishia maisha wafanyikazi wake kwenye gari waliomokuwa wakisafiria na kisha wakatoweka na kiasi hicho cha pesa. Hata hivyo wawili hao baadae walijitokeza na kukanusha madai ya kumuibia Promota huyo shilling laki 2 kwa kusema kwamba pesa hizo ni malipo ya performance yao lakini Eddie K Promotions amesisitiza kuwa lazima wasanii hao wamerejeshe pesa zake kwa kigezo kuwa hawakustahili kulipwa kiasi hicho cha pesa kwa performance yao mbovu waliyofanya.

Read More