Hanstone Aibua Madai Mazito Dhidi ya WCB Wasafi

Hanstone Aibua Madai Mazito Dhidi ya WCB Wasafi

Msanii wa Bongo Fleva, Hanstone, amevunja ukimya kuhusu maisha yake ndani ya lebo ya WCB Wasafi, akieleza hadharani changamoto alizokumbana nazo kipindi alichokuwa akihudumu humo. Akizungumza juzi kwenye mahojiano, Hanstone alidai kuwa alikaa ndani ya WCB kwa kipindi cha miaka mitatu bila kutambulishwa rasmi kama msanii wa lebo hiyo. Katika kipindi hicho, alieleza kuwa alihusika katika kuandika nyimbo kwa wasanii wengine, wakiwemo majina makubwa kama Diamond Platnumz, lakini hakuwahi kulipwa chochote kwa kazi hiyo.  “Nilitumika kuandika nyimbo kwa wasanii waliokuwa juu, lakini sikuwahi kupewa nafasi yangu wala stahiki zangu. Niliamini kwenye mchakato, lakini haikuwa kama nilivyotarajia,” alisema Hanstone kwa hisia. Kwa muda mrefu, mashabiki na wadau wa muziki wamekuwa wakimtaja Hanstone kama msanii asiye na subira, sifa ambayo imeonekana kuwa chanzo cha yeye kutopata nafasi ya kung’aa akiwa chini ya lebo hiyo ya WCB. Hata hivyo, msanii huyo amekana madai hayo, akisema alijitahidi kuwa mvumilivu, lakini hakupata fursa aliyostahili. Kauli ya Hanstone imezua mjadala mkubwa mitandaoni, huku baadhi ya mashabiki wakionesha huruma na kumuunga mkono, wakati wengine wakihimiza wasanii chipukizi kuwa na uvumilivu zaidi wanapojiunga na lebo kubwa kama WCB. Kwa sasa, bado haijajulikana ikiwa Hanstone atachukua hatua za kisheria au ataendelea na muziki kama msanii huru nje ya lebo hiyo. Mashabiki wanasubiri kwa hamu kuona hatua yake inayofuata.

Read More
 Hanstone adai kuibiwa wimbo na Diamond Platnumz

Hanstone adai kuibiwa wimbo na Diamond Platnumz

Msanii wa Bongofleva Hanstone ameibuka na madai ya kwamba Diamond Platnumz ameiba wimbo wake kwenye kazi yake mpya “CHITAKI” ambayo ameidokeza kwenye mitandao ya kijamii. Kupitia insta story yake, Hanstone ameanika wazi hilo kwa kuweka kipande cha wimbo wake uitwao “NATETEMEKA” ambapo kwenye file inaonesha aliufanya mwaka 2019. Utakumbuka Hanstone na Diamond walikuwa na ukaribu ambapo Hanstone alikuwa anatajwa kuwa angesainishwa na lebo ya WCB lakini baada ya kutokea utofauti wa pande zote mbili dili hilo lilitajwa halikuweza kukamilika.

Read More
 HANSTONE AACHIA RASMI THE AMAZING EP

HANSTONE AACHIA RASMI THE AMAZING EP

Msanii wa muziki wa kizazi kipya  nchini Tanzania Hassan Ramadhani Masanja maarufu kama ‘Hanstone’ ameachia EP yake mpya aliyoipa jina “The Amaizing” yenye jumla ya nyimbo 7. Mkali huyo ambaye alikuwa akihusishwa kuwa ni msanii mpya ajae kutoka lebo ya WCB, ameachia EP hiyo nje ya WCB. “The Amaizing EP” tayari inapatikana kwenye mitandao mbalimbali ya ku-stream muziki duniani. Hanstone ni mtoto wa pekee wa marehemu Banza Stone, alijipatia umaarufu kupitia ngoma ya Iokote aliyoshirikishwa na Maua Sama mwaka wa 2018.    

Read More