Happy C aumizwa na hatua ya Akeelah kuacha muziki.

Happy C aumizwa na hatua ya Akeelah kuacha muziki.

Msanii kutoka 001 music Happy C ameoneshwa kusikitishwa na kitendo cha Akeelah kutangaza kuacha muziki. Kwenye mahojiano na Captain Nyota amesema Akeelah ni msanii mwenye kipaji cha kipekee kwenye muziki wa Kenya, hivyo hapaswi kukata tamaa kwenye harakati za kuipambania ndoto yake kwa kuwa muziki una changamoto nyingi. Happy C amemshauri kujifikiria tena kutokana na maamuzi magumu ambayo ameyachukua kwenye muziki wake na atumie changamoto kama kigezo cha kufanya makubwa. Kauli yake imekuja baada ya Akeelah kusema ameamua kuacha muziki kwa sababu ya maonevu na unyanyasaji alioupitia katika safari yake ya mziki. Hitmaker huyo wa Tujikumbushe, alienda mbali Zaidi na kuushukuru uongozi wa Hakim Empire kwa mchango wao kwake huku akikosa kuutaja uongozi wa Shirko Media ambao ulimlea kimziki.

Read More
 Happy C aamua kuingia gym baada ya kuteswa na mapenzi

Happy C aamua kuingia gym baada ya kuteswa na mapenzi

Msanii kutoka lebo ya 001 Music Happy C amefunguka kwa mara ya kwanza kuanza mazoezi ya kuinua vyuma. Kwenye mahojiano na Lemmy Lito Sogohe, amesema imelazimika kuchukua uamuzi huo baada ya kuwa na msongo wa mawazo kutokana na kuvunjwa moyo na mpenzi wake. Happy C ameyalaani mahusiano ya mapenzi na kusema hakuna mapenzi ya kweli. Hata hivyo hajajulikana mrembo yupi huyo alimuumiza msanii huyo ambaye amekuwa akifananishwa na mwanamuziki wa Bongofleva Ali Kiba.

Read More
 MENEJA WA 001 MUSIC AKANUSHA HAPPY C KUUZA GARI KISA KUTOSWA NA JOHO

MENEJA WA 001 MUSIC AKANUSHA HAPPY C KUUZA GARI KISA KUTOSWA NA JOHO

Meneja kutoka lebo ya muziki ya 001 Music Mangisi amepuzilia mbali madai ya msanii Happy C kuuza gari lake baada ya walimwengu kuhoji ametoswa na bosi wa lebo hiyo Hassan Joho. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Mangisi amesema madai hayo hayana ukweli wowote kwani happy c bado anaendelea kupata msaada kutoka kwa gavana huyo wa zamani wa kaunti ya mombasa. Mangisi amekazia kuwa kuondoka kwa Hassan Joho mamlakani hautamrudisha nyuma kimuziki msanii Happy C kwa sababu ana imani kuwa Joho atamsaidia hata akiwa nje ya siasa. Kauli yake imekuja mara baada ya walimwengu kwenye mitandao ya kijamii kudai kuwa huenda Happy C ameuza gari lake kwani mara kwa mara amekuwa akitumia usafiri wa boda boda kwenye shughuli zake.

Read More
 HAPPY C AKANUSHA TUHUMA ZA KUIBA WIMBO WA HESHIMA

HAPPY C AKANUSHA TUHUMA ZA KUIBA WIMBO WA HESHIMA

Msanii kutoka 001 Music Happy C amekanusha madai ya kuiba idea ya wimbo wake mpya uitwao “Heshima” kutoka kwa Atumik wa leo. Kupitia ukurasa wake wa Facebook amemtaka Atumik akome kueneza taarifa za uongo kwamba alimuibia wimbo wa Heshima huku akimtaka msanii huyo aelekeze nguvu zake kwenye ishu ya kutangaza kazi zake za muziki badala ya kutengeneza mitukio ili azungumziwe na vyombo vya habari. Hata hivyo amesema anamheshimu Atumik kama mmoja wa mashabiki zake huku akiwataka wakenya waendelee kusapoti wimbo wake wa Heshima kwenye digital platflorms mbali mbali za muziki. Kauli ya Happy C imekuja mara baada Atumik wa leo kumtaka msanii huyo amlipe fidia kwa kuiiba ubunifu wake na kuutumia kwenye wimbo wake mpya Heshima  la sivyo atamchukulia hatua kali za kisheria.

Read More
 HAPPY C AACHIA RASMI BEYOND INFINITY EP

HAPPY C AACHIA RASMI BEYOND INFINITY EP

Msanii wa muziki kutoka 001 music Happy C ameachia rasmi EP yake mpya inayokwenda kwa jina la Beyond Infinity. Beyond Infinity EP ina jumla ya ngoma 5 za moto ambazo amewashirikisha wakali kama Chikuzee na K.O. EP hiyo ina nyimbo kama Yatakwisha, Inakera, Maupendo, Coco, na Heshima. Beyond Infinity inaenda kuwa EP ya pili kwa mtu mzima happy c ikizingatiwa kuwa mwaka wa 2021 aliwabariki mashabiki zake na EP iitwayo Karata 3 ambayo ilikuwa na jumla ya mikwaju tatu ya moto.

Read More
 MENEJA WA HAPPY C AFUNGUKA JUU YA UGOMVI NA MSANII WAKE

MENEJA WA HAPPY C AFUNGUKA JUU YA UGOMVI NA MSANII WAKE

Meneja wa msanii Happy C, Mwaringa amefunguka kwa mara ya kwanza kuhusu ugomvi wake na msanii huyo kutoka 001 Music. Katika mahojiano yake na podcast ya Captain Nyota, Mwaringa ambaye yupo chini ya Uptown Records amekiri kuwa Happy C alikuwa na deni lake kitu ambacho amedai kuwa lilimfanya kutokuwa na maelewano  mazuri naye ila kwa sasa wamezika tofauti zao baada ya Happy C kumlipa pesa zake. Mbali na hayo Mwaringa amedokeza ujio wa EP mpya kutoka kwa Happy C ndani ya mwaka huu EP ambayo kwa mujibu wake imekamilika kwa asilimia mia ila kwa sasa ni jambo la kuiachia tu. Hata hivyo amesema baada ya EP ya Happy C kutoka, kuna album ambayo pia itafuata ambayo kwa sasa inatayarishwa na chini ya prodyuza Totti. Utakumbuka juzi kati Mwaringa alitumia mtandao wake wa facebook kudai kwamba hajalipwa pesa zake na lebo ya 001 Music jambo lilompelekea kufuta video  zote za nyimbo za msanii wake Happy C youtube.

Read More
 HAPPY C ATANGAZA UJIO WA EP YAKE MPYA

HAPPY C ATANGAZA UJIO WA EP YAKE MPYA

Msanii wa muziki kutoka 001 music Happy C ametangaza ujio wa EP yake mpya ambayo ana mpango wa kuachia ndani ya mwaka huu wa 2022. Akiwa kwenye moja ya interview  happy C amewataka mashabiki wake kukaa mkao wa kula kuipokea EP yake hiyo ambayo kwa mujibu wake itakuwa na jumla ya mikwaju 5 ya moto. Hata hivyo hajeweka wazi jina la EP wala tarehe rasmi ambayo EP yenyewe itaingia sokoni ila amesema uongozi wake wa 001 music ndio utahamua siku ambayo EP yake hiyo itaachiwa. Hii unaenda kuwa EP ya pili kwa mtu mzima Happy C ikizingatiwa kuwa mwaka wa 2021 aliwabariki mashabiki zake na EP iitwayo Karata tatu ambayo ilikuwa na jumla ya mikwaju tatu ya moto.

Read More