HARMONIZE AIACHIA RASMI HIGH SCHOOL ALBUM
Baada ya listening party ya album mpya ya harmonize “High School” iliyofanyika usiku wa kuamkia leo kwenda vizuri, boss huyo wa Konde Gang, ambaye tayari ana miaka mitano tangu atoke na kutambulika rasmi kwenye muziki wa Bongo Fleva, ameichia rasmi album hiyo yenye jumla ya mikwaju 20 ya moto na collabo 6 pekee. Hitmaker huyo wa “Teacher” amewapa mashavu wasanii wageni kama rapa Sarkodie kutoka Ghana, Naira Marley kutoka Nigeria na Busiswa kutoka Afrika Kusini. Kwa upande wa tanzania wapo wakali kama Anjella, Sholo Mwamba na Ibraah ambao wanaikamilisha orodha ya kolabo kwenye album hiyo. Kwasasa “High School” inapatikana kupitia majukwaa mbalimbali ya ku-stream muziki mtandaoni. Hii itakuwa ni album ya pili kwa mtu mzima harmonize baada ya “Afro East” iliyotoka mwezi Machi mwaka wa 2020, ambayo ni miongoni mwa album kumi bora katika mtandao wa BOOMPLAY Afrika Mashariki
Read More