HARRY KANE MBIONI KUONDOKA SPURS

HARRY KANE MBIONI KUONDOKA SPURS

Imefichuka kuwa mshambuliaji wa  klabu ya Tottenham, Harry Kane, anajiandaa kuondoka zake baada ya klabu hiyo kumwajiri kocha mpya, Antonio Conte. Hayo yanasemwa huku Kane akisema Conte ni mmoja kati ya makocha bora duniani, ikiwa ni mara ya kwanza kwa mchezaji huyo kuzungumza tangu Tottenham ilipomtimua Nuno Espirito Santo. Mfungaji bora huyo wa Ligi Kuu England msimu uliopita, alikaribia kujiunga na Manchester City miezi michache iliyopita, kabla ya Mwenyekiti wa Tottenham, Daniel Levy, kuzuia uhamisho wake.

Read More