HART THE BAND WAONYA VIJANA DHIDI YA KUBUGIA POMBE KUPINDUKIA

HART THE BAND WAONYA VIJANA DHIDI YA KUBUGIA POMBE KUPINDUKIA

Wasanii wa kundi la Hart the band kutoka Kenya wamewaonya vijana dhidi ya kubugia pombe kupindukia. Wakizungumza moja kwa moja na Mpasho, wamesema vijana siku hizi wamekuwa waraibu wa kutumia vileo bila kuchukua tahadhari, jambo ambalo wamedai kuwa ni tishio kwa usalama wao ikizingatiwa kuwa wengi usahau kula na hata kuendesha magari kiholela wakiwa walevi. Katika hatua nyingine wamesema hawatumii ‘kiki’ kutambulisha kazi zao za muziki kwa sababu si aina ya maisha ambayo wamezoea tangu waanze muziki miaka kumi iliyopita. Wasanii hao ambao walilamba dili la ubalozi wa kinywaji cha Black & White wameongeza kuwa aina ya mashabiki wao pamoja na kazi zao nzuri za muziki wanazotoa pia huwafanya wasifikirie kabisa masuala ya kiki kama ambavyo hufanyika kwa baadhi ya wasanii hapa nchini Kenya.

Read More
 HART THE BAND WAACHIA RASMI ALBUM YAO MPYA

HART THE BAND WAACHIA RASMI ALBUM YAO MPYA

Kundi la muziki nchini Hart the Band limeachia rasmi album yao mpya iliyokuwa ikisubiriwa na mashabiki zao kwa muda. Album hiyo inayokwenda kwa jina la Party time ina nyimbo nane za moto ikiwa na kolabo 3 kutoka kwa wakali kama nyashinski, Alika na Phyl the kangogo. Party time album ina nyimbo kama Jienjoy, Na Bado, Sitaki Ma-Pressure, Easy like ABCD inapatikana exclusive kwenye digital forms zote za kupakua na kusikiliza muziki mtandaoni ikiwemo Boomplay, Sportify, Hustle sasa na nyingine nyingiu. Party time ni Album ya  tatu  kutoka kwa Hart the Band baaada ya, ‘Made In The Streets‘iliyotoka mwaka 2019 na ‘Simple Man’ iliyotoka mwaka 2021. Utakumbuka Hart The Band ni kundi la muziki kutoka Kenya na linaundwa na wasanii watatu ambao ni Mordecai Mwini Kimeu, Wachira Gatama, na Kenneth Muya Mukhwana.

Read More
 HART THE BAND KUACHIA ALBUM YAO MPYA MWISHONI MWA JUMA HILI

HART THE BAND KUACHIA ALBUM YAO MPYA MWISHONI MWA JUMA HILI

Kundi la muziki nchini Hart the Band limetangaza rasmi kuachia album yao mpya mwishoni mwa juma hili. Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa kundi hilo, limechapisha cover ya album yao kwa jina Party Time huku likisema album hiyo itatoka rasmi Mei 6 mwaka huu wa 2022. Party time album ina nyimbo nane za moto ikiwa na kolabo 3 kutoka kwa wakali kama nyashinski, Alika na Phyl the kangogo. Hii inaenda kuwa album ya tatu kutoka kwa Hart the Band baaada ya, ‘Made In The Streets‘iliyotoka mwaka 2019 na ‘Simple Man’ iliyotoka mwaka 2021. Utakumbuka Hart The Band ni kundi la muziki kutoka Kenya na linaundwa na wasanii watatu ambao ni Mordecai Mwini Kimeu, Wachira Gatama, na Kenneth Muya Mukhwana.

Read More
 H_ART THE BAND WATAMBULISHA COVER LA ALBUM YAO MPYA

H_ART THE BAND WATAMBULISHA COVER LA ALBUM YAO MPYA

Kundi la muziki nchini Hart the Band limetambulisha rasmi cover la album yao mpya iitwayo Party Time. Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa kundi hilo, limechapisha cover ya album yao huku likisema album hiyo itatoka rasmi Mei 6 mwaka huu wa 2022. Hii inaenda kuwa album ya tatu kutoka kwa Hart the Band baaada ya, ‘Made In The Streets‘iliyotoka mwaka 2019 na ‘Simple Man’ iliyotoka mwaka 2021. Utakumbuka Hart The Band ni kundi la muziki kutoka Kenya na linaundwa na wasanii watatu ambao ni Mordecai Mwini Kimeu, Wachira Gatama, na Kenneth Muya Mukhwana.

Read More
 H ART THE BAND MBIONI KUACHIA ALBUM YAO MPYA

H ART THE BAND MBIONI KUACHIA ALBUM YAO MPYA

Kundi la muziki nchini Hart the Band limetangaza ujio wa album yao mpya ambayo itaingia sokoni mwaka huu. Kupitia ukurasa rasmi wa Instagram wa kundi hilo, limetoa taarifa hiyo iliyoambatana na picha yenye ujumbe “NEW ALBUM LOADING” ikiashiria wapo kwenye maandalizi ya album mpya. Hii inaenda kuwa album ya tatu kutoka kwa Hart the Band baaada ya, ‘Made In The Streets‘ iliyotoka mwaka 2019 na ‘Simple Man’ iliyotoka mwaka 2021.

Read More