Mama Fina amkingia kifua mwimbaji wa Kadongo Kamu Hassan Nduga kwa tuhuma za wizi

Mama Fina amkingia kifua mwimbaji wa Kadongo Kamu Hassan Nduga kwa tuhuma za wizi

Mganga wa kienyeji kutoka nchini Uganda Mama Fina ameamua kumkingia kifua mwimbaji wa Kadongo Kamu Hassan Nduga baada ya kutuhumiwa kuhusika kwenye wizi wa pesa za kugharamia matibabu ya msanii Ronald Alimpa aliyehusika kwenye ajali mbaya ya barabarani wiki iliyopita. Mama Fina amenyosha maelezo kwa kusema kuwa hakumpa Hassan Nduga pesa za Ronald Alimpa kama inavyodaiwa bali alitoa shillingi laki 5 za kugharamia matibabu ya msanii huyo na akampa mama yake mzazi. Mwanamama huyo amesisitiza kuwa bado anaendelea kumtumia pesa za mahitaji ya msingi msanii huyo ambaye bado anauguza majeraha mabaya ya ajali. Kauli ya Mama Fina inakuja baada ya familia ya Ronald Alimpa kumchafulia jina Hassan Nduga kwa madai ya wizi wa shillingi laki 5 za kugharamia matibabu ya hitmaker huyo wa “Seen Don” alizopewa na mama Fina.

Read More
 Mwanamuziki Ronald Alimpa asikitishwa na waliofuja pesa za kugharamia matibabu yake

Mwanamuziki Ronald Alimpa asikitishwa na waliofuja pesa za kugharamia matibabu yake

Msanii kutoka nchni Uganda Ronald Alimpa ameonesha kusikitishwa na kitendo cha msanii mwenzake Hassan Nduga kuhusika kwenye wizi wa pesa za msaada alizopewa na wahisani kwa ajili ya kugharamia matibabu yake. Kwenye mahojiano yake hivi karibuni Alimpa amesema  msanii huyo alifuja takriban shillingi millioni 1.5 kati ya millioni 2 alizopokea kutoka kwa msamaria mwema kwa kigezo cha kugharamia mahitaji ya wasanii wenzake waliopata naye ajali wiki moja iliyopita. Hitmaker huyo huyo “Alimpa” ameenda mbali zaidi na kusema kuwa licha ya Nduga kumsaidia kipindi alihusika kwenye ajali ya barabarani hajafurahishwa na kitendo chake cha kuwatangazia watu misaada aliyokuwa anampa akiwa hospitalini. Utakumbuka Ronald Alimpa, Lady Grace na Ragga Fire walihusika kwenye ajali mbaya ya barabarani huko Ssemuto Katika wiliya ya Nasakeseke wiki moja iliyopita, lakini kwa bahati mbaya  msanii lady grace alifariki dunia papo hapo huku akiwaacha wengine na majeraha mabaya.

Read More